''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Monday, February 18, 2013

 UJUMBE WA JUMAPILI: MUNGU ANA MPANGO MZURI KWA AJILI YAKO
----------------------------------------------------------------------------------
MAANDIKO: Yeremia 10:23, Isaya 30:19-27
MHUBIRI: Mch Meshark Mhini
---------------------------------------------------

Mungu alikuumba sio kwa ajili yako mwenyewe bali ni kwa ajili yake hivyo basi mkabidhili leo mambo yako yote ili akuongoze kuyapangilia kwendana na mapenzi yake. Ni kweli unapitia mapito flani flani magumu lakini fahamu kuwa Mungu anafahamu kuwa unapitia katika hali hiyo, nab ado ana mpango mzuri kwa ajili yako labda anaruhusu hayo ili akutengeneze uwe chombo chake kizuri zaidi, kwahiyo usikate tamaa, kuwa mvumilivu, endelea kumuomba Mungu naye atafanya kitu kizuri sana kwa ajili yako zaidi ya kile ulichotegemea.
 Mungu ana mpango mzuri leo kwa ajili yako, mpango wa kukutana na shida zako zote. Hapo katika Isaya, Mungu aliwaambia wana wa Israel, ‘wewe hautalia tena’. Mungu anakwambia leo hautalia tena, usilie tena Mungu ana mpango mzuri kwa ajili yako cha muhimu, Kaa karibu na Mungu, Mwamini Mungu, Jitenge na uovu wa kila aina acha dhambi kabisa, na utambue wewe bila Mungu si kitu wala huwezi kitu.


No comments:

Post a Comment