''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

SISI NI NANI

---------------------------------------------------------------------------------------------------------


Tanzania Assemblise of God Mwenge ni kanisa la kiroho linaloongozwa chini ya Tanzania Assemblise of God (T.A.G).

Lipo maeneo ya Mwenge wilaya ya Kinondoni karibu kabisa na hospitali ya Mama Ngoma na maghorofa ya jeshi.

Kanisa la Mwenge ni mojawapo ya Makanisa ya mahala pamoja katika mtandao mkubwa wa usajiri wa T.A.G. Kitaifa. Mtandao wote toka ngazi ya mwanzo kupanda juu, utawala umegawanyika kwa ngazi zifuatazo; Sehemu, Jimbo, Kanda na hatimaye Kitaifa. Hivyo T.A.G. Mwenge iko sehemu ya Kinondoni, Jimbo la Mashariki. T.A.G. Kanisa lilianzishwa tarehe 27/12/1978. Hivyo Desemba 2008 lilitimiza miaka 30.
Historia ya T.A.G Mwenge inasimulika vizuri zaidi chini ya msingi imara wa utendaji wa Muasisi wake Rev. J. E. Mboma, ambaye aliyefariki Agosti 2006. Amerithiwa na aliyekuwa Mchungaji Msaidizi, Mchungaji Abdiel Meshack Mhini. 
Hivi sasa Kanisa linasonga mbele kama Jeshi la Mungu lililo imara.
Tuna ibada mbili ya kiingereza na kiswahili  ili kutoa fursa kwa watumiaji wa lugha zote mbili kumwabudu Mungu kwa uhuru na haki.

Kanisa lina wachungaji wasaidizi kama ifuatavyo; Mch. Musa Elias,  na Mch. Wiliam Nyimbi

Pia kuna balaza la wazee likiongozwa na mzee kiongozi Dr.Mughamba.

No comments:

Post a Comment