''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, January 7, 2019

SIRI YA KUTOA KWA AJILI YA KAZI YA MUNGU

Mhubiri: Ms. Irene Swai
Maandiko: 2Wakorintho 8:1-12

Watu wa Makedonia walikuwa ni watu wenye dhiki nyingi lakini walionyesha utofauti sana kwasababu pamoja na dhiki walizo nazo walitoa sana zaidi ya uwezo wao, walitoa sana kwajili ya kazi ya Mungu. 

Utoaji ni kipimo mojawapo cha upendo, ukimpenda sana mtu utajitoa sana kwa ajili yake, vivyo hivyo ukimpenda sana Mungu hutapata shida kutoa kwa ajili ya kazi yake. Watu wa Makedonia walimpenda sana Mungu ndomana hawakujali kuwa wana uwezo mdogo bali walitoa sana zaidi ya uwezo wao. Upendo ni tendo ni lazima ulionyeshe, huwezi ukasema unampenda sana Mungu alafu hujitoi wala hutoi kwa ajili ya kazi yake.

UTOAJI ni FURSA ya KUONYESHA UNAVYOMPENDA MUNGU. Mungu aliweka hili tendo la Utoaji ili tuweze kuonyesha jinsi tunavyompenda. Mungu amejikamilisha kila kitu na kila kitu ni vyake, Mungu alisema tumtolee sadaka si kwasababu hana, hapana bali ni fursa aliyotupa, Paulo anasema ni Neema. Kwahiyo toa pesa yako nguvu zako kwasababu ya Upendo wako kwa Mungu.

2Wakorintho 9:6-8,10-11 inaonyesha kuwa ni Yeye ndiye anayetupa nafasi ya kutoa, ni Yeye ndiye anayetupa mbegu ya kupanda ili tupande tuvune tumtolee kwa ajili yake. Yaani Yeye ndiye aliyesababisha ukapata hiyo kazi/biahsara uliyonayo inayokupa hela, sasa kwanini uwe mzito kumtolea Mungu? Kwanini uwe mzito kutoa kwa ajili ya Injili?

Huu ni mwanzo wa mwaka, kila mtu anapanga unapanga kwamba uendelee katika mambo yako fulani, lakini Je umepanga kwa kiasi gani unataka uongeze Upendo wako kwa Mungu? Je katika mwaka huu ni kwa kiasi gani umepanga kumtolea Mungu?

No comments:

Post a Comment