''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, January 13, 2019

JIPANGE UPYA KWENDA VIWANGO VINGINE!

Mhubiri: Mch. Kazimoto
Maandiko: Kutoka 31:1-6

Katika mwaka huu mpya, Jipange upya kwenda viwango vingine. Kuna kujipanga na kuna viwango vingine, kujipanga ina maana kuna mambo ulikuwa hujaweka sawa kwahiyo unayaweka sawa kwa kuyapanga vizuri kwa kuwa na mipango mizuri; na viwango vingine ina maana viwango ambavyo hukuvifikia mwaka jana kwahiyo mwaka huu mpya panga kuvifikia; kama mwaka jana ulikuwa unachelewa kanisani basi mwaka huu uwahi, kama mwaka jana ulikuwa mvivu katika kazi basi mwaka huu fanya kwa bidii. Huu ni ujumbe wa kiroho na kimwili pia. 

Katika kazi/biashara zako weka viwango vingine kuwa na ubunifu mwingine zaidi kuliko mwaka jana, ukifanya mbinu zilezile za mwaka jana hutaweza kupata matokeo mapya, kama unataka maendeleo zaidi kuliko mwaka jana badilisha mbinu ulizotumia mwaka jana, tafuta mbinu nzuri zaidi kupata matokeo mazuri. Roho Mtakatifu aingie kwako aweke ubunifu kila kona, akikupa ubunifu kila kona maendeleo yatakuja pesa itakuja utaendelea kiroho na kimwili. Kutoka 31:1-6, Mungu ameweka akili nyingi sana ndani mwako ni wewe tu kuitumia.Huu ni mwaka mpya weka viwango vipya vya kiroho na kimwili.

Ili uweze kuendelea mbele hatua za muhimu kuliko zote ni; 

1. MUWEKE MUNGU AWE NAMBA MOJA(1) KWENYE MAISHA YAKO. Tunavyosema Mungu awe namba moja maana yake ni umpende kuliko kitu chochote kile, inamaana maombi upo, mikesha upo mifungo upo, usiweke mambo mengine mbele kuliko Mungu, MUngu awe namba moja kwanza kuliko vitu vyote, kwa ambaye hujaokoka uokoke, kwa ambaye ulilegea utengeneze maisha yako na Mungu, na kwa uliye vizuri jitahidi usirudi nyuma. 

2. Achana/ vunja vitu vyote vinavyo kurudisha nyuma; kama ni tabia flani, kama ni maagano flani ulifanya ya ukoo vunja vunja yote kwa Jina la Yesu. Gideon kabla hajaenda viwango vingine aliambiwa avunje miungu ya wazazi wake ili apande viwango vingine.
- Kuna vitu ambavyo usipovipinga hutaweza kuendelea, kama ukiangalia kwenye ukoo unaoona kuna ngome ambao inazuia anza mara moja kuivunja. Kama ukijiangalia unaona umeokoka vizuri lakini bado huendelei, je unazani ni kwanini ipo hivyo? hapo kutakuwa tu kuna kitu kimejificha amua kufanya maombi ya vita na kuvunja kila kitu cha shetani
- Kuna vitu usipotoa katika maisha haiwezekani kwenda hatua nyingine.
- Ili kutoka katika maisha ni lazima uchukie hali uliyonayo.

No comments:

Post a Comment