''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, January 27, 2019

WEKA MTAZAMO MPYA SASA

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Hosea 4:6

Hosea alikuwa na ujumbe mkubwa sana wa kuwaonya watu wale lakini watu wale  kwasababu ya mtazamo wao mbaya hawakuusikia. Njia pekee ya kuwa na mtazamo mpya na wa uhakika ni kwa kupata maarifa ya Mungu, na maarifa hayo utayapata kupitia Neno la Mungu. Fahamu kuwa ni muhimu sana sana kuwa na mtazamo sahihi na ulio safi.

Sahivi ni mwanzo wa mwaka, weka mtazamo mpya sasa, usirudie rudie mipango yako ya jana, weka mipango mipya, mfano; Jinsi gani wewe binafsi utasoma Biblia kwa uaminifu katika mwaka huu? Je umepanga kuomba kwa kiasi gani katika mwaka huu.

Ukisema umeokoka alafu husomi Neno la Mungu utakuwa unakosea sana. Jinsi Neno la Mungu linavyoweza kubadilisha mtazamo;
- Neno la Mungu linaongoza maisha,  wakristo wengi sasa hawana Neno la Mungu, kwahiyo wanadanganywa sana kwa kukosa maarifa.

No comments:

Post a Comment