''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, February 3, 2019

JIPE MOYO, WEWE NI MSHINDI!

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Warumi 8:28

Unaweza pitia mambo mengi magumu na ukaona kama mambo hayaendi lakini kumbuka kuwa hicho ni kipindi kifupi tu kitaisha na Mungu anasema anafanya kazi na wampendao.

 Warumi 8:28 "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake."

Dawa kubwa ya changamoto zinazokusumbua ni Maombi tu, Muombe Mungu bila kukata tamaa, Omba Omba Omba!. Ukisoma kuhusu Danieli utaona kuwa alimuomba Mungu bila kukata tamaa kwa siku 21 mpaka jibu lilipokuja. Maombi ni Suluhisho la kila tatizo, amini tu.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika maombi yako:
1. Maombi yako ni lazima yaongozwe na Neno la Mungu
2. Unapoomba ni lazima uombe kwa Bidii na kwa kumaanisha, Luka 6:13 Yesu alikuwa na Bidii ya maombi.
3. Ni Muhimu sana kuomba kwa KUNENA, 1Wakorintho 14:18
4. Kwenye maombi yako uwe unamsikiliza Roho Mtakatifu, maombi ni mawasiliano ya pande mbili, baada ya kumwambia haja zako ni lazima usikilize Roho Mtakatifu naye anasemaje, tenga muda wako mzuri wa kutulia na Mungu.

No comments:

Post a Comment