''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, February 17, 2019

BIDII YA UTOAJI HUSABABISHA MAONO

Mhubiri: Meja Daniel Long'way 
Maandiko: 2Nyakati 34:1-18

Katika hili Neno tunaona makuhani walipokuwa wakikusanya sadaka mara wakaona kitabu cha torati. Nikajiuliza hivi kuna uhusiano gani kati ya hela iliyokusanywa na kitabu cha torati?, yani kwanini kitabu cha torati kilionekana baada ya sadaka kutolewa, kwanini haikuonekana kabla? jibu la maswali hayo ndio ujumbe wa Leo, "BIDII YA UTOAJI HUSABABISHA MAONO". 

Mungu anawapa maono watu ambao wana maono kwa ajili yake, katika Neno tulilosoma wana wa Israel walikuwa wana maono ya juu ya nyumba ya Bwana, na Bwana naye akaamua awaonyeshe kitabu cha torati ili watambue dhambi walizonazo na kutubia, na baada ya pale utaona kwamba haikuongelewa tena kwamba ile pesa ilitumikaje bali habari ya kitabu cha torati.

Kuna uhusiano mkubwa kati ya bidii ya utoaji na maono, 1Wafalme 3:4-5 "4 Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile. 5 Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe." 

Baada ya Mfalme Suleiman kutoa sadaka elfu ndipo Bwana akamwambia "Omba Chochote", hata wewe ukitathimini zile siku ulizotoa kwa bidii Mungu alikupa maono ya kufanikisha maono yako, alifungua njia fulani. Ukitoa kwa bidii Mungu anafungua njia za tofauti sana zaidi ya unayodhani.

Mungu kipimo chake ni BIDII, kwendana na kiasi ulichonacho ukitoa kidogo kwa Mungu utapata maono madogo na ukitoa kwa kujidhabihu yani kwa bidii sana kwendana na uwezo wako Mungu naye atakupa maono makubwa sana.

Ukiwa pale nyumbani baba akileta mchele hawezi kusema leo familia yangu nimewafadhili mchele, hapana huko sio kufadhili maani lile ni jukumu lake, lakini unapotoa pesa kwa ajili ya kanisa la Bwana unakuwa umemfadhili Mungu na ukimfadhili Mungu, Mungu naye atakufadhili sana sana; Zaburi 18:25

Mungu akikupa shughuli ya kuifadhili ujue alishaona uwezo unao ndomana anataka umtolee ili baraka zije kwako

No comments:

Post a Comment