----------------------------------------------------------------------------------------------------
JINA LA YESU KRISTO – MOJAWAPO YA FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI
Na.Mwl.Mwakasege:
“Nami nakuambia ….. na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mathayo 16:18 – 19).
Maneno haya ya Yesu Kristo yanatuonyesha kuwa, nia yake ni kulijenga kanisa lililo na mamlaka kuliko shetani. Kanisa ni mwili wake (Waefeso 1:22 – 23). Wakristo waliookolewa kwa damu ya Yesu Kristo ni viungo vya mwili wa Kristo – ni viungo vya kanisa (1 Wakorintho 12:12, 13, 27). Kwa hiyo Yesu Kristo anaposema atalijenga kanisa lake wala milango ya kuzimu haitalishinda – ana maana ya kuwa, kila mkristo aliye wake anajengwa kiroho awe na mamlaka ya kumshinda shetani.
Ni budi tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufungue kama hakuna kitu cha kukifungua. Hawezi kutuambia tufunge kama hakuna kitu cha kufunga. Kwa hiyo ni lazima kuna vitu vya kuvifunga na kuna vitu vya kuvifungua.
Pia, tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufunge na kufungua kabla hajatupa uwezo na mamlaka ya kufanya hivyo. Uwezo na mamlaka tunapata ndani ya Kristo aliyetukabidhi funguo za ufalme wa mbinguni.
Itakuwa haina maana kwa Yesu Kristo kutukabidhi funguo bila ya kutufundisha namna ya kuzitumia. Hawezi kutukabidhi mamlaka bila kutufundisha namna ya kuyatumia.
Yesu Kristo anasema tukifunga au tukifungua, mbinguni nako kunatia mhuri kitendo hicho. Hatuwezi kufanya hivyo kama tulichokifanya hakifanani na mapenzi yake. Ndiyo maana tunaomba kuwa mapenzi yake yatimizwe hapa duniani, kama yanavyotimizwa huko mbinguni. Kwa maneno mengine tunaweza kusema ya kuwa ukifanya kitu chochote katika mapenzi ya Mungu, Ufalme wa mbinguni utakuwa upande wako.
------------------------------------------------------------------------------------------------------
NAMNA YA KUMSIFU NA
KUMWABUDU
MUNGU
Tumejifunza
mambo mengi sana yaliyokuhamasisha na yaliyokupiga deni uwe kiumbe wa kumsifu
na kumtukuza Mungu. Tunapomsifu mtu, huwa tunaelezea yale ambayo
yanamtofautisha na wengine. Hivyo basi, ufikapo katika muda wa kumsifu na
kumwabudu Mungu, ujue namna ya kuifanya sifa yako na ibada yako kwa usahihi.
Na ili kumpa Mungu sifa na
ibada, ni lazima na ni muhimu sana ujue mambo ambayo yanamstahilisha Mungu wetu
kusifiwa na kutukuzwa. Kwa kutumia sifa na tabia za Mungu, utaweza kumsifu na
kumwabudu vizuri. Hakuna kiumbe
kingine chochote kinazo zile sifa kuu tano za Mungu, isipokuwa yeye Mungu
Jehova peke yake.
Kwahiyo, na hizo ndizo zinayomstahilisha yeye kusifiwa na viumbe wake.
Katika sura ya nane, tumeshajifunza mambo yanayomstahilisha
Mungu kupewa sifa. Kwakuwa sasa unayajua, basi tumia mambo hayo uendapo mbele
za Mungu katika katika ibada yako ili kumsifu na kumwabudu. Unapomueleza Mungu
sifa zake na tabia zake (vile alivyo) hapo unakuwa unamsifu na kumwabudu.
Tofauti
ya kusifu na kuabudu
Naomba
urudie kuisoma sura ya kwanza ya kitabu hiki, ambapo nimefundisha vizuri maana
ya kumshukuru Mungu, kumsifu Mungu na kumwabudu Mungu. Hii itakusaidia
kutofautisha mambo haya kwa nia ya kuyaelewa au kuyaelezea kwa mtu mwingine.
Nilisema hivi,
Ibaba ni kitendo cha mtu kumtukuza, kumhimidi, kumwinua,
kumwadhimisha, kumshukuru na kumheshimu Mungu kwa vile alivyo na kwa yale
aliyoyatenda. (Appreciation and admiration for who God is and
for what He has done). Lakini haya mambo
matatu, yanayofanana sana na si rahisi sana kuyatenganisha kimaelezo au
kivitendo.
Lakini tuendapo mbele za Mungu
kwa ibada, iwe ni chumbani kwako au sebuleni kwako au kwenye gari lako au
kanisani kwako, kusifu na kuabudu na kushukuru, ni mambo yanayofanyika kwa
kuingliana sana. Sio sheria kwamba, hautakiwi kuchanganya sifa na kuabudu na
kushukuru, hapana. Hebu soma tena sura ya kwanza vizuri. Kati ya mengi,
nilisema hivi;
Haya mambo matatu, kusifu, kushukuru na kuabudu, ni mambo yanayofanana sana. Inaweza
ikawa vigumu kidogo kuyatenganisha kimaelezo au kivitendo. Ni ngumu kidogo,
kufanya kimoja pasipo wenzake, kwasababu ni mambo yanayokwenda kwa pamoja sana.
Lakini kwa tafsiri zake, yako hivi;
1.
Kumshukuru
Mungu;- Ni ile hali ya kumueleza Mungu jinsi tunavyothamini (Appreciate and Admire) wema wake, fadhili zake na
baraka zake katika maisha yetu.
2.
Kumsifu Mungu; - Ni kumueleza Mungu juu ya matendo yake makuu na ya ajabu aliyoyafanya. Au ni kuwaeleza wengine kuhusu matendo makuu ya
Mungu aliyoyafanya katika maisha yetu au kwa watu wengine.
3.
Kumwabudu Mungu; - Ni kumueleza Mungu tukuzo zetu, heshima yetu na upendo
wetu kwake kwasababu ya uzuri wa tabia zake kwetu.
(Credentials and Characters).
Kwahiyo,
tuendapo mbele za Mungu kwa ibada, iwe ni chumbani kwako au sebuleni kwako au
kwenye gari lako au kanisani kwako, ili kumsifu na kumwabudu na kumshukuru
Mungu, uwe huru kujimimina mbele za Mungu kwa kufanya vyote vitatu, kwa namna
moyo wako utakavyokuwa unaongozwa na Roho Mtakatifu. Vyote vitatu vinatengeneza
ibada takatifu kwa Mungu.
Katika sura inayokuja,
nimefundisha vizuri namna ya kuingia katika ibada na hata kupenya na kufika
katika chumba cha ndani kabisa cha uwepo na utukufu wa Mungu; ili unapokwenda mbele za Mungu wetu, uweze kukutana na nguvu zake
katika utukufu wake.
Lakini hapa chini nimeziweka kwa ufupi ili kukukumbusha. Na pia
nimekuongezea na mambo mengine yanayotakiwa katika kumsifu na kumtukuza Mungu.
Kwahiyo, utengapo muda wa kukaa mbele za Mungu wetu kwa ibada, msifu na
kumtukuza Mungu kwa mambo yafuatayo,
1.
Mtukuze Mungu kwa Sifa zake za Uungu
(ambazo hakuna mwingine aliye nazo) Kwamba;
a) Jehova
ni Mungu wa Milele
b) Jehova
ni Mungu Mtakatifu
c) Jehova
ni Mungu Aliye kila mahali
d) Jehova
ni Mungu Anayejua mambo yote
e) Jehova
ni Mungu Aliye na nguvu zote na
anaweza kufanya mambo yote
kabisa.
Nimezielezea vizuri hizi sifa za Uungu, katika
sura ya kwanza. Hizi ni baadhi tu ya sifa za Mungu, sio zote. Kwa hivyo basi,
pamoja na namna nyingine ambazo utajifunza kumsifu na kumwabudu Mungu, hebu uwe
unamsifu Mungu kwa mambo haya au kwa sifa zake hizi pia.
Msifu Mungu kwa;
2.
Kwasababu
ya Tabia zake
3.
Kwasababu
ya Matendo
yake ya Ajabu
4.
Kwasababu ya Fadhili nyingi na kuu mno
5.
Kwasababu
ya Ahadi
zake kubwa za thamani
2. Mtukuze Mungu kwa Tabia zake
Neno la Mungu, linatuonyesha jinsi ambavyo Mungu
wetu ana tabia na kawaida nyingi nzuri ambazo kwa hizo, tunavutiwa na tunapigwa
deni kumsifu na kumwabudu. Kwa mfano ; Biblia inasema kwamba, Mungu wetu
amejaa Upendo, usio na mwisho. Ni Mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, sifa
yake ni kuwa na rehema daima. Soma mistari ifuatayo, ili uone zaidi. Lakini
kwasababu ya sifa hizi (Tabia zake), tunapigwa deni kumsifu na kumwabudu.
*Zaburi 103:8, Kutoka 34 :6,
*Efeso 3 :18-19, Daniel 9 :4, Ufunuo
19 :11
3.
Mtukuze
Mungu kwa Matendo yake ya ajabu.
Mungu wetu ni Mungu aliyefanya mambo ambayo hakuna
tena, awezaye kufanya. Kwa mfano; ndiye aliyeziumba na kuzitundika sayari zote
za ulimwengu huu, bila minyororo wala nguzo. Mungu wetu ndiye anayesababisha
mioyo yetu inadunda, bile kuwekewa betrii wala chaji (charge). Au ni lini
ulichomeka moyo wako katika soketi ya umeme kama unavyochomeka simu yako ili kupata
umeme?
Nina uhakika, hakuna mtu anayefanya hivyo.
Sasa unadhani moyo wako unadundaje? Hizo ni kazi za ajabu za Mungu wetu.na
hakuna mtu awezaye kuzifanya. Kwasababu ya matendo yake ya ajabu, Mungu wetu
anastahili kusifiwa na kutukuzwa. Soma mistari ifuatayo kwa umakini. Utaweza
kuona kwa uchache, jinsi maandiko yanavyoeleza juu ya matendo makuu ya Mungu.
Haya ni maelezo ya watu wa Mungu ambao kwa kumjua
Mungu, waliweza kueleza ukuu wake vizuri, ili na sisi tunaosoma maandiko yao,
tunajifunza juu ya ukuu wa Mungu, uweza wa Mungu na tabia za Mungu wetu. Soma
vizuri Kitabu cha Daniel 6:25-27,
Nehemia 9:6, Zaburi
147:1-18, na Zaburi sura ya 136:4-26
4. Mtukuze Mungu
kwa Fadhili zake.
Mungu wetu ni Mungu atupaye baraka na fadhili
nyingi kila siku. Fikiri wema ambao Mungu amekufanyia maishani mwako, na hata
katika siku ya leo tu. Kuna vingi ametupa ambavyo wengi walitamani, lakini
hawakupewa. Uhai, afya, ulinzi, rehema, chakula, fedha, shule, simu, gari,
nyumba, ajira, mke, mume, watoto, na hata wazazi.
Sio kila mtu bado ana wazazi. Na wengine wamezaliwa hawajawahi kuwajua
wazazi wao. Kwakweli fadhili na baraka za Mungu ni nyingi sana; ukiamua
kuziorodhesha, utakesha. Sasa, kwa fadhili zote hizi alizotujalia, basi Mungu
wetu anstahili kusifiwa.
*Zaburi 103:1-5,
Zaburi 107:21, 2Nyakati 20:21
5.
Mtukuze Mungu
kwa
Ahadi zake.
Ni
Mungu aliyetuahidi watu wake, mambo mengi sana mazuri. Ametupa ahadi kubwa mno
na za thamani sana. Ni ahadi za kutupa baraka, heshima na utajiri. Kwa ahadi hizi
pia, anastahili kusifiwa * 2Petro
1:3-4, Efeso 1:3-4, Kumbu 4:4-8
Kwa ufupi, hivi ndivyo unavyotakiwa kumsifu na kumwabudu Mungu. Kadri
unavyoanza kufanya hivi kwa vitendo, utaendelea kujifunza kufanya huduma hii
ipasavyo, nawe utajikuta unakutana na nguvu za Mungu kwa namna ya tofauti
maishani mwako.
MSIFU MUNGU KWA MAJINA YAKE.
Majina ya Mungu, hueleza sifa za Mungu, Tabia za
Mungu au Matendo ya Mungu. Mfano; Wayahudi wanamwita Mungu El-Shaddai. Ni neno lenye
majina mawili ndani yake. ‘El’ maana yake Mungu, na ‘Shaddai’ lenye maana itokanayo na
neno ‘Shad’
yaani Titi (Ziwa) la mama
anyonyeshaye.
Kutokana na ukweli kwamba, titi/ziwa la
mama anyonyeshaye, linampa mtoto mchanga kila kitu anchohitaji. Maziwa ya mama
yake, humpa mtoto kila kitu mtoto anachohitaji. Ndani ya maziwa kuna vitamini,
protini, wanga, mafuta, madini, maji, na kila kitu mtoto anachohitaji. Maziwa
ya mama, yanamtosheleza mtoto kwa kila kitu. Hivyo, Waisraeli
wanapomwita Mungu El-Shaddai, wanamaanisha kuwa, kama ziwa linavyo mtosheleza mtoto, vivyo hivyo, Mungu
ni ‘Mtoshelezi’ kwetu.
Halleluyah!
Hivyo, kila jina la Mungu, linabeba
aidha Sifa yake au Tabia yake au Matendo yake. Ndio maana Mfalme Daudi anasema
“Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu … Mpeni
Bwana utukufu kwa jina lake. Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.” (Zab 29:1-2) Msifuni Bwana
kwa kuwa Bwana ni mwema, Liimbieni
Jina lake, kwakuwa lapendeza.(Zaburi 135:3).
Na Bwana Yesu alitufundisha kuanza sala namna hii;
Baba yetu uliye
mbinguni, jina lako tukutuzwe,
hakafu Ufalme wako uje hapa duniani.
Kwahiyo,
unaweza pia kumsifu Bwana kwa majina yake. Majina ya Mungu, hueleza aidha sifa za Mungu au tabia za
Mungu au Matendo makuu ya Mungu. Yafuatayo hapa chini, ni
baadhi ya majina ya Mungu kwa lugha ya Kiebrania, yatakayokusaidia kumsifu,
kumwabudu na kumshukuru Mungu.
MAJINA YA MUNGU
Jina
la Mungu Maana yake Mstari wa Biblia
1.
Adonai - Mungu Mwenye enzi yote - Mwa 15:2-8, Kut 6:2-3
2.
El-Ohim
- Mungu Muumbaji - Mwa 33:20, Kol 1:16-17
3.
El-Elyon - Mungu Aliye juu zaidi - Mwa14:18, Dan 4:34
4.
El-Gibbor - Mungu
Mwenye Nguvu - Isa 9:6,
Zab 147:5
5.
El-Hai
- Mungu Aliye Hai/Anaishi -
Josh 3:10, 1Sam17:26
6.
El-Olam - Mungu wa Milele - Ufu 4:8,
Kut 3:14
7.
El-Roi - Mungu Aonaye kila kitu - Mith 15:3, Zab 32:8
8.
El-Shaddai - Mungu
Mtoshelezi - Mdo 17:28, Kumb 8:4
9.
Jehovah - Ajitegemeaye kuwepo -Kut
6:2-8, Mdo 17:24-25
10.
Jehovah Shalom -Mungu Amani yetu - Amu
6:22-24
11.
Jehovah
Rapha -
Mungu Atuponyaye
- Kut 15:26
12.
Jehovah
Jireh -
Mungu Mtoaji wetu - Mwa 22:
8, 14
13.
Jehovah Nissi -
Mungu Ushindi wetu -
Kut 14:13-14
14.
Jehovah Saboath -
Bwana wa Majeshi - Malaki 3:7
15.
Jehovah Shammah - Bwana ni Aliyepo -
Kut 3:14
16.
Jehovah Rohi -
Bwana ni Mchungaji wangu - Zab 23:1
17.
Jehovah Tsidkenu -
Bwana ni Haki yetu -
Yer 23:6
18.
Jehovah Mekaddishem -
Bwana Atutakasaye - Kut 31:13
Namna za
kumshukuru, kumsifu, na kumwabudu Mungu wetu.
Kwahiyo, katika maisha yetu sisi, kama waumini,
tunatakiwa kumpa Mungu wetu ibada, (kumshukuru, kumsifu na kumwabudu) kwasababu ya mambo yote hayo
niliyoyataja. Tunatakiwa kumtukuza Mungu kwasababu ya sifa zake, na kwasababu
ya tabia zake, na matendo yake na fadhili zake na ahadi zake kwetu.
Sasa basi, hapa chini, nimekuwekea njia
kuu tatu ambazo unaweza kumsifu na kumtukuza Mungu kwazo. Utengapo muda wa
kwenda mbele za Mungu, unaweza kutuia njiia kuu zifuatazo; Kumtukuza Mungu kwa,
- Kumwimbia nyimbo za kumsifu na kuwabudu
- Kumweleza au kusimulia kwa maneno
- Kumtolea Mungu sadaka na dhabihu
Wako katika kazi ya Mungu
Mwl.
Mgisa Mtebe
+255 713 497
654
mgisamtebe@ yahoo.com
www.mgisamtebe.org
somo la muhimu sana kwa kanisa la leo
ReplyDeleteamina
ReplyDeleteAme asante kwa ujumbr
ReplyDelete