''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, November 26, 2017

NGUVU YA KANISA LINALO OMBA

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Matendo 1:4-14, 12:5-9

Kanisa linaloomba ni kanisa linalotegemea kurudi kwa Yesu, Ni kanisa linalotegemea nguvu ya Roho Mtakatifu. Kanisa linaloomba linatarajia kitu. Tujifunze kutoka kanisa la Kwanza. 

Agizo la Bwana Yesu kwa wanafunzi wake lilikuwa ni kumsubiri Roho Mtakatifu ndipo kuanza kazi ya kumtumikia Mungu. Kanisa lisiloomba huwa na malumbano bali kanisa linaloomba huwa na umoja na nguvu. Kanisa linalodumu katika maombi ibilisi hawezi kuingia wala kukaa humo.

Asili ya kanisa lenye nguvu ni kudumu katika Maombi. Kanisa lisilodumu katika maombi shetani hujenga makao ndani yake na hakutakuwa na nguvu ya Mungu. Tarajia kitu katika kanisa linaloomba. Watu wote katika Biblia waliokuwa wakiomba kwa bidii matokeo yake yalionekana.

Kuomba kuna faida, katika Matendo 12:5-9 Petro alifunguliwa toka katika kifungo kupitia maombi ya kanisa lililoamua kuomba kwa ajili ya Petro. Yoshua alikuwa ni kamanda wa vita na kwa kutulia nyumbani mwa Bwana aliwashinda wa amaleki. Yoshua alitulia hemani kwa Bwana kumuomba Mungu nyakati zote naye Mungu hakumuacha.

Mtu wa Mungu yakupasa kukaa katika maombi muda wote ili upate nguvu ya Mungu katika maisha yako itakayo mshinda yule mwovu. Petro Minyororo ilikatika kwa sababu kuna watu walikuwa wanaomba. 

Kanisa La Mungu lapaswa kutulia katika Maombi na kudumu humo. Lazima maombi yaendelee ndani ya kanisa la Mungu wakati wote na hakuna kikomo cha Maombi. Sasa ni wakati wa kuwa Imara katika Maombi. Achana na Kukimbia Maombi na kuwaachia watu wengine, wote tuliookolewa ni waombaji.

Huwezi kuwa Hodari kama huombi.

No comments:

Post a Comment