''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, December 3, 2017

BARAKA KAMA MAFURIKO

Mhubiri: Mch. Kitoi
Neno: 2Timotheo 4:9-14

Kwa kupitia Musa, Bwana Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka utumwani, ilipawapasa wamsikilize Bwana sana aliyewatoa Misri lakini pia na kuambatana na Musa ambaye alikuwa anapokea maagizo kutoka kwa Mungu. Moja ya kitu ambacho kinaweza kufanya ukabarikiwa sana ni kumjali mchungaji wako, mtumishi wa Mungu anayekuchunga.

Mambo Muhimu ya kufanya ili upate baraka
1. Shikamana na Mchungaji wako mpaka mwisho.
2. Jijenga tabia ya kumtembelea mchungaji wako nyumbani kwake.
3. Jijengee tabia ya kumpa Mchungaji wako fedha mara kwa mara.

Ndani ya Mchungaji kuna baraka zote za kiroho na za kimwili. Mchungaji kazi yake kubwa ni kutamka baraka. Neno la mchungaji ni la muhimu sana kwako, fanya kitu kwa mchungaji wako, mchungaji akikiona akukumbuke, wewe kukumbukwa na mchungaji hata kama asipokuombea hiyo ni kitu kikubwa sana.

Ili uendelee kupata baraka kama mafuriko ni lazima usiache imani, ni lazima uzingatie wokovu wako. Mungu ana kanuni zake ili baraka ziendelee lazima uzingatie kanuni hizo. Lakini pia ni lazima uwe na mahusiano mazuri na Mungu, unajua pesa sio kitu cha kwanza bali mahusiano yako na Mungu ndio kitu cha kwanza. Mahusiano yako na Mungu yanapokaa vizuri mipango yako yote itafanikiwa.

No comments:

Post a Comment