''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, December 10, 2017

KAZA MACHO YAKO KWA YESU

Mhubiri: Mch. Abdiel Mhini
Maandiko: Waebrania 12:1-3, 4:14-16

Mateso ya mwenye haki yalisaababishwa na dhambi iliyotendeka huko nyuma, lakini wewe kama mwenye haki hutakiwi kukata tamaa. Unatakiwa umtazame Yesu, ukaze macho yako kwa Yesu. Yesu ndiye wakili wako anayeweza kukusaidia na kukutetea.

Mashahidi ni wale tuliowasoma kwenye Biblia waliopata mateso mengi lakini hawakumuacha Mungu. Kwahiyo Neno hili linatutia moyo sisi tulio sasa, kwamba tusimuache Yesu tumtazame Yeye tu. Haijalishi una hali gani hata kama una hali mbaya sana cha kufanya wewe ni kutulia kwa Yesu, mtazame Yesu tu!, muombe Mungu kwa bidii na Mungu atatenda tu. Unajua Mungu anakupenda sana, yawezekana unaomba kitu fulani miaka na miaka huoni jibu, lakini bado Neno linasema tumtazame Yesu, usikate tamaa ipo siku utapata jibu lako. Yesu yupo na Yesu atajibu tu, ipo siku shida yako Yesu ataiponya.

Mathayo 5:10, Heri waliyovumilia shida zote bila kumuacha Yesu, ndugu yangu Yesu yupo upande wako.

Mambo mawili  ya msingi
1. Wewe ni mshindi kwa kupitia jina la Yesu.
2. Amini kuwa Yesu anaweza, na kuwa na muda wa kuomba, tunaposema mtazame Yesu haimaanishi uangalie tu bali uwe unaomba.
3. simama imara na mtegemee Yesu.

1cor 10:13, Kila jaribu Mungu anaweka mlango wa kutokea, Mungu ni mwaminifu hawezi kukuacha ukajaribiwa zaidi ya uwezo wako. Mungu akubariki.

No comments:

Post a Comment