''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, December 17, 2017

KUABUDU KATIKA ROHO NA KWELI

Mhubiri: Mr. Elisha Suku
Maandiko: Yohana 4:7-24

KUABUDU ni nini, kuabudu kwa maana rahisi ni kumpenda Mungu, kumpa Mungu utukufu heshima anayoshahili, na kumtii Mungu. Na hapa Yesu anazugumzika kuabudu katika Roho na Kweli. Anamwambia mwanamke wa Kisamaria muda umebadilia watu hawatamwabudu Mungu Yerusalem au mlimani bali katika Roho na Kweli.

Huwezi kumwambudu Mungu katika roho na kweli kama huna Yesu ndani mwako, kwasababu Yesu ndio aliyerudisha ule uhusiano ambao ulipotea baada ya mwanadamu kutenda dhambi. Kwahiyo ni ndani ya Yesu TU ndio unaweza kumwabudu Mungu katika roho na kweli.

Mambo muhimu ya kuzingatia:

1. Mungu anatafuta wanao abudu katika roho na kweli (waabuduo halisi).
Na kama Yesu anasema "Waabuduo Halisi" inamaanisha kuna waabuduo wasio halisi. Unaweza ukazani unamwambudu Mungu lakini kumbe haumwambudu Mungu katika roho na kweli.  Kwahiyo ni jukumu lako mimi na wewe kuamua kuwa Waabudu Halisi,  na ili uwe Mwabudu Halisi lazima uwe na mahusiano hai na Yesu, lazima uokoke maana bila Yesu huwezi.

2. Mungu ni Roho, sasa ili tumwabudu lazima tumwabudu katika roho. Mungu ambaye yupo katika roho inaamisha yuko sehemu yote, huwez ukasema wewe ni Mwabudu Halisi wakati unamwambudu Mungu kanisani tu alafu nyumbani na kazini huwezi kumwambudu. Mungu yuko sehemu yote unaweza ukamwabudu sehemu yoyote hata njiani, kwenye gari n.k. Nyumbani kwako ukipata tu sehem ambayo haina usumbufu unaweza kuabudu. Lakini pia hata ukiwepo kanisani wepo kwa kumaanisha, kuna wengine wanakuwepo kanisani lakini akili zao hazipo kanisani, anawaza vitu vya nyumbani kwake alafu badae anasema kwenye ibada hajapata kitu, sasa swali ni je Yeye aliweka akili yake tayari kuabudu?. 

Je kuna maana gani ya kumwabudu katika roho?
Kwenye Yohana 3:5-6, kilichozaliwa na roho ni roho, sasa mtu uliyeokoka umezaliwa mara ya pili katika roho. Kwahiyo ili umwabudu Mungu katika roho ni lazima uzaliwe mara ya pili katika roho. 

Je kuna maana gani ya kumwabudu katika kweli?
Yesu ndiye kweli

Warumi 12:1-2, Lazima ujitoe mwenyewe kama dhabihu na kuacha kufwatisha namna/ mambo ya dunia hii ili kuweza kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli. Kwahiyo tunagundua kwamba kumwabudu Mungu ni maisha, sio kitu cha siku moja tu au muda wa kanisani tu. Ili kuwa mwabudu wa kweli lazima maisha yako uyatoe kwa Mungu, kuyatoa inamaanisha kujitenga na namna ya dunia hii. Mfano Wakati wa sasa ukifungua hata simu kwenye mitandao kuna mambo mengi machafu yanayoendelea ambayo lazima uamue kuyaacha kama kweli unataka kuwa mwabudu halisi mwenye uhusiano hai na Mungu. Mungu akusaidie umwambudu katika Roho na Kweli.

No comments:

Post a Comment