''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Monday, January 1, 2018

NAMNA YA KUYAUMBA MAISHA YAKO, KWA MWAKA 2018

Mhubiri: Mch. Mussa Elias
Maandiko: Mwanzo 1:1- 2:4

Ni namna gani unaweza kuyapa sura maisha yako. Andiko hili Mungu anaweka kama mfano wa kazi, Mungu kila alichokuwa anakifanya alikuwa ana pangili na kupanga muda kamili.
Mungu wetu ni Mungu wa mipango, na wewe mwanzo wa mwaka huu 2018 weka malengo yako na jinsi ya kuyafikia. 

Jinsi ya kuyaumba maisha yako, ni lazima uyaangalie maisha yako kwenye mtazamo mpya, una shida gani kwenye maisha yako na tumia hizo shida zako kuwa fursa kwa kutafuta jinsi ya kuyatatua. Hapa tuliposoma Mungu anaanza kwa kuonyesha shida ambayo hakupenda iendelee (Ukiwa na Utupu), hali ambayo Yeye haikumfurahisha jinsi kulivyokuwa, ndiomana akaanza kuumba kwa kutamka na iwe nuru. Kwahiyo hata wewe labda kuna hali flani ambayo haikupendezi, basi tamka kile unachotaka kiwe. Mungu anavyosema alituumba kwa mfano wake na kwa sura yake, inamaanisha na wewe una uwezo wa kuumba una uwezo wa kutamkia maisha yako kitu na kikawa, kemea matatizo kwa Jina la Yesu nayo yataondoka.

Watu wengi hawaendelei kwasababu hawaoni tatizo kama ni fursa na kibaya zaidi wengine wanaona matatizo ndio kitu cha kuwaambia wengine. Hiyo sio 'style' ya Mungu wetu.  Ukiwa na tatizo sio muda wa kunyong'onyea bali kubali tatizo lako alafu weka mpango wa kulitatua.

Lakini, pia tunajifunza Mungu alikuwa na tabia ya Kujitathimini, huwezi kusema umemuona Mungu wakati hupigi hatua, bali ili useme umemuona Mungu ni lazima uwe na malengo, panga malengo yako ya mwaka huu alafu muombe Mungu, ukifikia malengo yako hapo ndio umemuona Mungu. 

Mungu alianzia mbali alikuwa na 'vision' (maono) alitaka duniani kuwe sehemu nzuri kwa ajili ya mwanadamu, na akaanza kutekeleza, akaona hili giza litoke kuwe na mwanga n.k

Zab 5:4-6, mwaka huu tembea kama mtu unayefahamu nafasi yako, mtawala, ukikuta shida weka mipango tekeleza tatua tatizo.

Dondoo za kujifunza kutoka Mwanzo 1
  1. Tunaweza kuwa na mipango hata wakati usioofaa, kati ya vitu visivyofaa visivyo na matumaini, Mwanzo 1:2  
  2. Tumeona mwanzo Roho alikuwa ametulia juu ya maji, sasa tunajifunza Roho Yeye huwa yupo tu anasubiri umpe kazi ya kufanya, kwahiyo usipoweka mipango yako Roho Yeye atabaki tu ametulia kwasababu Yeye ni msaidizi sasa kama huna kazi nakuwa hana cha kukusaidia.
  3. Elewa kwa UHAKIKA (exactly) unachotaka kwenye maisha, Mungu alitaka dunia nzuri kwahiyo ALIANZA KWA "KUTAMKA" na Roho akaanza kufanya kazi.
  4. Mungu alitaka vitu vizuri, na wewe penda kitu chako kiwe vizuri.
  5. Ukikataa maarifa Mungu hawezi kufanya kazi na wewe.
  6. Mungu aliumba vitu kwa majira na wakati, kwahiyo na wewe jifunze kufanya vitu kwa 'timing' 
  7. Mungu alikuwa na muda wa kutathimini alichokifanya, na ili utathimini ni lazma uwe na malengo ili ujue hili vizuri hili vizuri kidogo, Mungu alitathimini kila siku baada ya kazi (process evaluation) na tathimini ya jumla.
  8. Alisherekea mafanikio yake, kwahiyo ni lazima na ni kiMungu kusherekea mafanikio/ kufikia malengo uliyopata

No comments:

Post a Comment