''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, November 19, 2017

JIPONYE NAFSI YAKO USITAZAME NYUMA

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Mwanzo 19:1-22, Ufunuo 3:15-17, 
Luka 17:32-33, Zaburi 119:113, Yakobo 1:7-8, 
Luka 21:34-36

Lutu alikuwa mwenyeji wa Sodoma. Malaika wa Bwana walikuja kwa Lutu na kumwambia kwamba atoe yeye na ndugu zake nje ya mji maana Mungu anataka kuuangamiza mji wote. Lutu alitii na kwenda kuwaambia familia yake lakini hawakuelewa kwa haraka mpaka malaika akawashika mkono na kuwatoa. 

Malaika alivyowatoa familia ya Lutu akawaga agizo Mwanzo 19:17 ( 17 Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea), Kwamba wasitazame nyuma lakini mkewe Lutu alitazama nyuma na matokeo yake aligeuzwa kuwa nguzo ya chumvi. 

Neno hili linatufundisha kwamaba tusiangalie nyuma. Bwana Yesu anasema kwenye kitabu cha Luka kwamba tumkumbuke mkewe Lutu kwamba aliangalia, akasema kwamba yeyote atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza na yeyote atakayeiangamiza ataiponya. Shetani kazi yake ni kukukumbusha yale uliyoyafanya wakati wa dhambi ili uyakumbuke na kuyarudia ila ujumbe huu unakukumbusha kwamba usiangalie nyuma.

Kushindwa kufuata mambo ya Mungu na kuyafuata yale ya dunia ni kuangalia nyuma,  na unaweza ukawa umeanza kuangalia nyuma kwa njia ya kawaida sana, kwa mfano; kwenda kwenye mechi ya mpira ukaacha ibada ni kuangalia nyuma. Hiyo ni mojawapo ya mifano, hali yoyote ya kuweka kitu cha kwanza zaidi na Mungu kumuweka nafasi ya pili na kuendelea hicho ni kiashiria cha kujijua kwamba umeacha kugeuka.

Lakini neema bado ipo mpaka sasa, kama umeangalia nyuma muda wa kutubu ni sasa maana yeye hupokea mtu anaerudi. Amua kurudi sasa na uache dhambi zote zilizokuwa zinakurudisha nyuma, uanze na Bwana.

No comments:

Post a Comment