''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, May 26, 2013

KINGA YAKO AU TEGEMEO LAKO NI NINI?MAANDIKO: Yeremia 17:5-8
MHUBIRI: Mrs. Subira Mitimingi(Mama Mch. Mitimingi)

Yeremia 17:5-8; “5. Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. 6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.
8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.”
Biblia inaweka wazi kuwa anayemtegemea mwanadamu amelaaniwa, kwahiyo tambua kwamba ukimtegemea mwanadamu tu utakuwa umejipatia laana papo hapo. Amua leo kumtegemea Mungu na kumfanya awe kinga yako. Mungu si kama mwanadamu, mwanadamu ni kigeugeu, mwanadamu ana kikomo.

Kwahiyo usikubali ngugu yangu kutegemea mwanadamu kwasababu utakuwa unatembea na laana.Mungu hampendi mtu anayemtegemea mwanadamu, ukimpenda mwanadamu Mungu anajitoa ndani mwako anakaa pembeni. Lakini tambua kuwa Mungu akijitoa katika maisha yako, ulinzi wa maisha yako utaondoka kwahiyo shetani atapata nafasi ya kukutesa kadiri anavyotaka.

Siku za leo, kuna baadhi ya watu wanaamini kwamba uponyaji unapatikana katika kanisa flani au kwa mchungaji flani au mchungaji flani akikuombea ndo utapona au mpaka uende kuombewa kanisa flani ndo utapona, Nakutaarifu kuwa hutapona wala hutapata Baraka wala mafanikio kwa njia hiyo bali utajiongezea laana kwasababu huko ni kumtegemea mwanadamu kuliko Mungu au huko ndo kulitegemea kanisa flani kuliko Mungu, na Biblia inasema  amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu, kwahiyo utakuwa umelaaniwa papo hapo. Ndugu yangu amua leo kumtegemea Mungu tu!.

Pia, ukimtegemea mwanadamu Mungu huondoa hazina yake iliyo ndani mwako, mfano kama ulikuwa ni mwimbaji mzuri karama ile ya uimbaji itaondoka na utaanza kuimba vibaya.
Ukimtegemea mwanadamu utakuwa unakaribisha roho ya ufukara katika maisha yako(angalia mstari wa 6)

Hata siku moja usiseme bila flani mimi siwezi kufanya kitu flani, mfano mtu aliye na huduma asiseme bila mtu flani huduma hii haitaweza endelea au bila flani huduma hii isingekuwepo, eti kwasababu anachangia pesa nyingi au kwa kiasi kukumbwa. Kama utasema hivyo ipo siku Mungu atamtowesha mbali huyo mtu anayechangia sana ili upate shida umkumbuke Yeye.

Ukimtegemea mwanadamu, utakuwa na maisha ya uchungu kwasababu Baraka za Mungu zitaondoka  hazitakufuata.

Ndugu yangu tambua hili, Baraka za Mungu zinatakiwa ziwe zinakufuata na sio wewe uzifuate. Watu wengi sasa wanahangaika huku na kule kisa wanatafuta Baraka/ kubarikiwa, kwa njia hiyo ndugu hutapata Baraka za kweli, Tenda haki Baraka zitakufuata popote ulipo, Yeremia 17:8.

Mfalme Suleimani alimtegemea Mungu akapata Hekima ya Ki-Mungu, Mfalme Daudi pia alimtegemea Mungu akaweza kumuua goliati kwa kajiwe kadogo. Kwahiyo siri kubwa ni kumng’ang’ania Mungu tu.

Vitu vyako vingi haviendi kwasababu unategemea akili zako mwenyewe au unamtegemea mwanadamu mwenzako. Amua leo kumtegemea Mungu acha kujitegemea, kutegemea pesa au mwanadamu.

No comments:

Post a Comment