''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, July 21, 2013SOMO: JE NI SIKU NGAPI ZA KUSAFIRI KWAKO?
MHUBIRI: DR. MUMGHAMBA
Kutoka 14:10-31, 15:1-13 

Je ni siku ngapi za kusafiri kwako? Wana wa Israel walitumia miaka 40 kutoka misri mpaka kanani, daudi naye alipoulizwa umri wake hakusema miaka yake bali alisema muda wa kusafiri kwake, maisha ya kiroho/ya wokovu ni safari,  je ni siku ngapi za kusafiri kwako na katika safari hiyo umeona nini?

Wana wa Israel waliona Mkono Mkuu wa Mungu katika Kutoka 14:31 “Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya Bwana juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha Bwana, wakamwamini Bwana, na Musa mtumishi wake.” Wana wa Israel waliona mkono wa Mungu ukiwapigania na ukawasaidia wakavuka bahari ya shamu, walitazama kushoto na kulia kulikuwa na milima nyuma jeshi la farao linakuja mbele bahari lakini mkono wa Bwana tu ndio uliowaokoa

Wewe je umeona nini? Je umeona matendo makuu ya Mungu?, katika Yeremia 1:11-12, Yeremia aliulizwa na Mungu Yeremia waona nini? Akasema naona ufito wa mlozi Ndipo Bwana akamwambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.

No comments:

Post a Comment