''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, March 13, 2016

KURUDISHA HESHIMA YAKO NA YA KANISA

Mhuiri: Mch. Lauden Mwafongo (kutoka mbeya)
Maandiko:1Samweli :17:40-54


UTANGULIZI
Ili heshima yako irejee ni lazima goliati aanguke lakini pia ili goliati aanguke lazima Daudi ainuke. Daudi ni mtumishi wa Mungu aliyepakwa mafuta ili kurejesha heshima ya wanaisraeli na uzao wao wote. Ili Daudi aweze kuirejesha heshima ya Mungu wa Israel ilibidi aamue kwa kujiamini kwenda kupigana na goliati aliyeharibu heshima hiyo.

Baada ya Daudi kupakwa mafuta  alijawa na upako wa Mungu uliyofanya yeye kurudisha heshima yake na ya wana wa israeli. UPAKO ni uwezo wa MUNGU unaoachiliwa kwa mtu wa MUNGU akafanye vitu kwa uwezo wa ki-Mungu.

Upako ni uwezesho wa Mungu ili ketenda yale yasiyowezekana kwa hali ya kibanadamu. Kitakachokuwezesha katika kila kitu utakachokifanya ni UPAKO na bila huo huwezi kufanya lolote.

Kurudisha heshima sio kazi ndogo inahitaji nguvu ya ziada na ndio maana YESU alipoondoka aliwambia wanafunzi wake kuwa wasifanye lolote pasipo uweza toka kwa Baba(MUNGU)
Kinachomtofautisha aliyeokoka na asiyeokoka ni UPAKO ndani ya mtu/ kanisa(kinachotutofautisha ni nguvu ya MUNGU katikati yetu.

BAADA YA MTU WA MUNGU KUPAKWA MAFUTA NA MUNGU HUFANYA MAMBO HAYA.

1.Unafanyika mtu mwingine, 1Samweli 10:1
Utakapopakwa mafuta ya ki-Mungu utageuzwa kiroho na MUNGU mwenyewe. Kitakachofanya kanisa la MUNGU liwe tofauti ni nguvu za BWANA. Ukibadilika kiroho utafanya mambo yasiyo ya kawaida, mfano; Samsoni alipobadilika baada ya kupakwa mafuta ya ki-Mungu alifanya mambo yasiyo ya kawaida. Elia pia vivyo hivyo. YESU naye alipokuja duniani alifanya mambo yasiyo ya kawaida na sisi pia tunaweza kufanya mambo yasiyo ya kawaida iwapo tutakubali kuishi chini ya nguvu za Mungu. UPAKO unafiti kila eneo.

2.Wanaleta Mageuzi.
Watu wa Mungu huleta mageuzi na wala wao hawageuzwi kokote pale. Daudi alipoenda kambini aligeuza hali ya pale na kumpiga goliati bila yeye kubadilishwa. Pia Lazima tuangushe madhabahu zote zisizo za ki-Mungu kwa kuwa sisi ni wana mageuzi. Fanya mageuzi kila mahali tangu nyumbani kwako hata kazini na mahali pote(Mfano Danieli alipofanya mageuzi katika Falme ya ulimwengu). SISI NI WANA MAGEUZI NA NI LAZIMA TULETE MAGEUZI POPOTE TULIPO
Wewe sio wa kawaida na ni wa pekee na maisha yetu ni ya pekee. Yesu pekee atatufanya tuwe wazuri kuliko vitu vyote duniani.

3.Wanajua kwa nini wapo pale na wanamtumikia MUNGU katika Roho na kweli.
katika kazi ya MUNGU haina utani-utani kabisa!. Ukijaa upako wa Mungu unapofika mahali pa kutumika kwa ajili ya utukufu wa MUNGU.

UNAPOPEWA NAFASI NA MUNGU UMTUMIKIE BASI MTUMIKIE MUNGU KWA MOYO WAKO WOTE NA NGUVU ZAKO ZOTE NA AKILI ZAKO ZOTE PASIPO KULETA UTANI KATIKA KAZI YA MUNGU.

No comments:

Post a Comment