''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Thursday, April 7, 2016

NGUVU YA KITABU HIKI

Mhubiri: Dkt. Mchungaji Peter Mitimingi
Maandiko: Yoshua 1:8

Yoshua 1:8
"kitabu hiki cha Torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapostawi sana."

Musa alifanya kila kitu kwa kutumia nguvu iliyokuwepo nyuma ya fimbo lakini Yoshua alifanya kila kitu kwa kutumia nguvu iliyopo ndani ya Kitabu.

Baadhi ya Matukio Ambapo Mungu aliitumia Fimbo ya Musa kufanya maajabu.

1.    Fimbo ya Musa yaleta Vyura Juu ya Nchi - Kutoka 8:5-6
2.    Fimbo ya Musa yabadili Mavumbi kuwa Chawa - Kutoka 8:16 -17
3.    Fimbo ya Musa yaleta Nzige katika Nchi - Kutoka 10:13
4.    Fimbo ya Musa yagawanya Bahari ya Shamu - Kutoka 14:16
5.    Fimbo ya Musa yaleta Ushindi Vitani - Kutoka 17:9
6.    Fimbo ya Musa yatoa Maji kutoka katika Mwamba - Kutoka 17:5-6

Mungu Badala ya Kuendeleza Matumizi ya FIMBO kwa Joshua anaamua kubadilisha mtindo kutoka kwenye fimbo  kwenda Kwenye KITABU/NENO LA MUNGU


Baadhi ya Matukio Ambapo Mungu aliitumia KITABU kwa Yoshua Kufanya Maajabu.

1. Yoshua anatumia Kitabu kinywani mwake kukausha mto Yordani ili watu waweze kuvuka-Yoshua 3:16

2. Yoshua anaangusha ukuta wa Yeriko kwa kutumia Kitabu (Kelele) Yoshua 6:5-6

3. Yoshua hakutumia fimbo kusimamisha jua, alitumia NENO/KITABU alichopewa - Yoshua 10:13


NGUVU 10 ZA KITABU HIKI

1. Ni Kitabu Cha Tofauti Kuliko Vitabu Vyote.

2. Ni Kitabu Chenye Majibu Ya Maswali Na Matatizo Ya Aina Yoyote Katika Ulimwengu Huu.

3. Ni kitabu kinacho badilisha maisha ya watu walioshindikana na kuwafanya waweze kuwa watu wazuri na wengine kuwa watumishi. 

4. Ni Kitabu Kinachowafanya Watu Waliokuwa Wazuri Waweze Kuwa Bora Zaidi. Mfano: Kornelio Matendo 10:44 - 45

5. Ni Kitabu Kinachowapa Wanadamu Dira Na Kuwaelekeza Njia Sahihi Ya Kufika Mbinguni. Zaburi 119:105

6. Ni Kitabu Kinachotoa Amani Ya Kweli Isiyoweza Kupatikana Mahali Pengine Popote.

7. Ni kitabu Pekee Chenye Pumzi ya Uhai Ndani Yake. Waebrania 4:12
"Maana Neno la Mungu li hai,tena lina nguvu,tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili,tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho,na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake;tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo."

8. Ndicho Kitabu Pekee Kisichopitwa Na Wakati Kuliko Vitabu Vyote Duniani.

9. Ni Kitabu Pekee Chenye Uwezo wa Kuponya Magonjwa ya Mwili na Roho. Zaburi 107:20, Mathayo 8:8, Zaburi 147:3

10. Ni kitabu Pekee Chenye Uwezo wa Kukaa Kwenye Moyo wa Mtu. Zaburi 119:11
"Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi."

No comments:

Post a Comment