''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, May 15, 2016

TUNAZO NGUVU ZA MUNGU ZILIZO ZAIDI YA NGUVU!!

Mhubiri: Mch. Ambele Chapanyota
Maandiko: Hesabu 23:23-24

"23 Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
 24 Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba mke, Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hata atakapokula mawindo, Na kunywa damu yao waliouawa".

Sisi ni watoto wa Ibrahimu na ndIo maana tunaishi kwa imani tukimwamini YESU KRISTO kuwa ni mwana wa MUNGU na anayo mamlaka yote. Tunapoishi kwa imani kumwamini
Yesu basi tunakuwa ni watoto wa ahadi ndani ya Kristo. "HAKUNA MUNGU MWENYE NGUVU DUNIANI KAMA MUNGU WETU". Hivyo mimi na wewe tuna nguvu za MUNGU ndani yetu na hakuna anayeweza kutushinda. Hakuna nguvu itakayokushinda kwa kuwa una nguvu za MUNGU asiyeshindwa na chochote.

Petro na Yakobo walikuwa ni watu wa kawaida kama wewe lakini nguvu ya MUNGU iliposhuka juu yao walibadilishwa na kuwa watenda miujiza, hata kama upo katika shida ya aina gani nguvu ya MUNGU ikishuka lazima utainuka na utachanua maana nguvu ya MUNGU imeshuka.

"UNAZO NGUVU ZAIDI YA NGUVU KWA KUMWAMINI MUNGU NA KUMWABUDU". Hatuwezi kuwa wa kawaida maana tuna nguvu ndani yetu isiyo ya kawaida. Hata kama tumekosa vitu vingine lakini kama tuna YESU sisi si wa kawaida. Usidanganyike na Wachungaji wanaokwambia ulete chumvi na vitu vingine hao wote ni waongo mwamini MUNGU aliyekuokoa tu na Uombe kwa bidii.

Ukiisha kuokolewa tu na MUNGU umeingia katika ukoo wenye nguvu ya MUNGU aliye juu mbinguni aliyetuokoa. YESU anacho cheo chako kwa sababu ya nguvu inayopatikana kwa YESU.

No comments:

Post a Comment