''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Thursday, August 24, 2017

UTAKATIFU NA UTAKASO

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: 1Petro 1:2, 1Petro 2:11-12

Kila mtu aliyeokoleawa amaetakaswa na damu ya Yesu, tangu siku ile ulitakaswa na damu ya Yesu. Sasa kama ulitakaswa na damu ya Yesu ni lazima uendelee kuwa msafi. Kujitakasa na utakatifu zinatakiwa ziwe ni tabia zako za kila siku. Ili uweze kuendelea kuwa mtakatifu ni lazima uwe unasoma Neno kila siku na kuomba, ni lazima mahusiano yako na Mungu yawe mazuri.

Unapojazwa na Roho Mtakatifu unakuwa umetakaswa, lakini kwa bahati mbaya wengi wetu wameangalia nyuma wamerudi nyuma. Nakushauri ndugu yangu usirudi nyuma, wewe jali sana utakatifu wako. Wewe kama uliyeokolewa hutakiwi kabisa kufanya dhambi, na hapa ukumbuke kuna dhambi zile za siri ambazo unaona au unajua hakuna mtu anayekuona, lakini kumbuka Yesu anakuona na alishakutakasa, kwahiyo acha kabisa hizo dhambi. Kama wewe sio mwaminifu kwa mume au mke wako acha kabisa hiyo tabia. Ni vyema ukatubu sasa, hujui kwanini ujumbe huu unauona sahivi ni afadhali ukachukua hatua. Hatuji kanisani kama maonyesho au hatuokoki kama maonyesho, acha dhambi, madhara ya dhambi ni mabaya sana, usifanye dhambi.

1Petro 2:11-12, Hili ni onyo maalumu kwa kanisa, acha dhambi, dhambi ni mbaya, hizi ni siku za mwisho. Matamanio ya kufanya dhambi yameongezeka, kwanini unazani unapata hamu ya kufanya dhambi ni kwasabbabu umemuacha Mungu, umeacha kusoma Neno la Mungu na kutumia muda wako kuomba.

1Petro 4:1, Yesu aliteswa kwa ajili yako ili wewe uweze kuwa mtakatifu, kumbe Yesu alipata shida kwa ajili yako. Sasa kama unatambua kazi aliyoifanya kwanini unarudia tena dhambi au kwanini unamuacha? Mruhusu Yesu afanye makazi ndani yako ili aweze kukupa uwezo wa kushinda dhambi.

Warumi 6:1-2; sasa je kwasababu wakati huu neema ipo, ndo uzidi kufanya dhambi?, hapana acha dhambi, huwezi jua Yesu anakuja lini, kuwa mwaminifu kwa mke/muwe wako lakini hata ambao hawajaoa kuweni waaminifu msifanye dhambi mbele za Mungu.

No comments:

Post a Comment