''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, August 4, 2013

NJIA/NAMNA YA KUFANYA UMISHENI

MHUBIRI: Mch. Abraham Masasi.
 
1. MTU MWENYEWE KUTOKA NA KWENDA KWENYE ENEO LA INJILI
Hii njia sio ya kukurupuka ni mpaka usikie wito wa Mungu kutoka moyoni, unatakiwa uwe na uhakika kama kweli Mungu amekuita na sio kubahatisha. Matendo 20:22, Ukijigundua kama una wito huo nenda kwa mchungaji wako na umwambie kuhusu hilo. Umisheni wa namna hii inahitaji Mungu aseme na wewe juu ya kwenda mahali flani kupeleka injili

2. KUOMBA KWA AJILI YA UMISHENI
Ni muhimu sana kuwaombea wale walio katika maeneo ya umisheni katika nchi mbalimbali. Ni Lazima uombe kwa ajili ya wamishionari. Tunapaswa kuombea maeneo hayo watu watakayo kwenda kufanya huo umisheni, Mungu awaokoe na kuwafungua wale watu wanaopelekewa Injili. Pia kuwaombea kwa dhati hao watakaoenda(wamishionari) kufanya kufanya umisheni, Mungu awape kibali mbele ya watu wa eneo hilo la umisheni.

  Paulo aligundua hilo ndomana hakuwaomba watu pesa lakini aliwaomba waendelee kumuombea, Matendo 15:30-31. Kibali cha Mungu ni cha muhimu sana maishani mwetu, Mungu awasaidie wamishionari wapate kibali mbele ya jamii na mazingira hayo mapya watakaoenda. Paulo hakujivunia kwamba anajua kuzungumza bali alinyenyekea kwa Mungu na kuwaomba wamuombee apate kibali mbele za watu. Ukitaka kipawa chako kikue au huduma yako ikuwe rudi kwa Mungu, nyenyekea mbele zake na sio kujisifu, Luka 10:2



3. KUTOA
Inatupasa sisi kuwapeleka kwa kutoa fedha zetu, Luka 10:14-15, kuna makudi mawili kuna wale wanaoenda kwenye maeneo ya umisheni yaani wamishionari na kuna wanaowapeleka wale wamishenari. Toa sadaka kwa Bwana kutoka moyoni yaani kwa moyo wa kupenda.
Huwezi kutenganisha umisheni na utoaji. Efeso 6:15-16, Huduma ya umishionari inahitaji fedha nyingi, wamisionari wakienda kwenye maeneo ya umisheni wanatakiwa wawe na pesa za kutosha. Hivyo basi jitaidi uchangie pesa nzuri ya umisheni, wamishionari hawa huwa wanaenda na familia zao kwahiyo inabidi pesa iwepo ya kuwalipia ada watoto wao na gharama nyingine zote za maisha. Karibu sana Mwenge TAG uwakilishe mchango wako wa Umisheni.

                                                         Mch. Abraham Masasi
                                                      

 

No comments:

Post a Comment