''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, August 11, 2013


SOMO: MALAIKA MMOJA KUTOKA KWA MUNGU
MHUBIRI: Mr. Frank Mwalongo
MAANDIKO: Mathayo 27:62-66,28:1-6 

Huyu ni yule malaika aliyekwenda kaburini wakati wa Yesu kufufuka. Yesu alivyokuja duniani aliacha aliacha utukufu na enzi akajifanya si kitu ili kwamba wokovu upatikane(Wafilipi 2:7). Sasa baada ya kufa Yesu, mafarisayo walimfuata pilato kumueleza habari ya kuwa Yesu alisema kuwa siku ya tatu atafufuka kwahiyo akawaamuru kaburi lilinde na maaskari kwasababu walihisi labda wanafunzi wake watakuja kumtorosha, kumbe hawakujua Yeye wanayemlinda ni Yesu, Yesu ambaye ni Mungu, Yesu ambaye ni mwokozi na hawakujua kwamba mipango yake binadamu hawezi kuzuia.

Kwahiyo askari wakaendelea kulinda kwa umakini sana lakini wakati ulipofika, siku ya 3, Mungu alimtuma malaika tena mmoja tu sio wawili wala watatu alishuka malaika mmoja tu huyo alitosha kumaliza kila kitu, Aliposhuka tetemeko la ardhi lilitokea likidhihirisha Nguvu za Ki-Mungu alizokuwa nazo, wale askari wakakamavu kabisa hawakuweza kustahimili wakaanguka na kuwa kama watu waliokufa wala malaika hakupigana nao alivingirisha jiwe alafu akakaa juu ya jiwe. Biblia inatuelezea kabisa kuwa malaika alikaa tu juu ya jiwe, lakini hakuna askari aliyeweza kuamka wakati wa ule uwepo wa malaika. Uwepo wa Mungu ukiwa ndani yako ni silaha tosha dhidi ya shetani, wala hataweza kukushambulia, kwasababu akipigana nawe atakuwa anapigana na Mungu.

Leo hii baba yangu, mama yangu, kaka yangu, na dada yangu, haijalishi una shida gani, hata kama una ugonjwa sugu ulioshindikana hospitalini, hata kama una shida kubwa kiasi gani, Mwambie Mungu Yeye ni yule yule jana leo na hata milele, Mungu atatuma malaika wake, naye atashuka na kuja kukaa kwenye shida yako nayo itakuacha, hatuitaji malaika wengi mmoja tu anatosha. shetani amekuwekea jiwe kubwa mbele yako usifanikiwe, jiwe la mateso, jiwe la dhiki na mengine mengi, mueleze Mungu sasa naye atatuma malaika nazo shida zako hazitaweza kusimama mbele yake zitatoweka ghafla, nawe utakuwa huru.




No comments:

Post a Comment