''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, August 18, 2013

LEO MWENGE TAG..

UJUMBE: MSAMAHA NA KUACHILIA
MHUBIRI: Mchungaji Mhini

Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.” Marko 11:25-26. Hapo ni Yesu Kristo akisisitiza msamaha, Unatubu sana lakini mungu hakusamehi kwasababu hauja msamehe mwenzako.

Yawezekana uligombana na kaka au dada yako au wazazi wako au ndugu zako, au ulimkopesha mtu pesa yako na mpaka leo hajakurudishia au mtu alikuaidi kitu cha muhimu na mpaka leo hajakitimia kwahiyo umebaki na ule uchungu ndani ya moyo wako, wasamehe sasa kwasababu bila msamaha Mungu hatakusikia mpaka uwasamehe na kuomba toba ndipo atakusikia.

Samehe ndugu yangu, Yawezekana kabisa wewe ni mwamini yaani umeokoka lakini kuna mtu unaishi nae au unafanya nae kazi au unasoma nae lakini hamuongei na pindi unapomuona kabisa hauna amani nae, msamehe mtu huyo leo. Yesu Kristo anasisitiza kuhusu msamaha, samehe leo ndugu yangu ili uwe huru moyoni. Itakuwa ni vyema kwako hivi leo kupiga moyo konde na kusamehe na kumsamehe kabisa huyo mtu/watu

Inawezekana unaweka sana bidii katika biashara yako lakini haupati faida nzuri au unafanya kazi kwa bidii lakini hauendelei au unasoma kwa bidii lakini haufanikiwi, kumbe ni kwasababu kuna mtu haujamsamehe kwahiyo ukimuomba Mungu akuwezeshe na kukufanikisha Mungu hakusikii kwasababu hujasemehe

Na inawezekana mwenzako amekuwa akikukosea mara kwa mara mpaka unahisi kama huna hamu tena ya kumsamehe, lakini bado Yesu anakusihi kwamba uendelee kumsamehe mtu huyo. Luka 17:3-4 “Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.”

Samehe leo ndugu yangu na Mungu atakusamehe, tubu mbele za Mungu na usirudie tena kufanya dhambi.

 
Watu wakijikabidhi kwa Bwana na Kusamehe wale walio wakosea

Watu wakitubu dhambi zao baada ya kasamehe walio wakosea

No comments:

Post a Comment