''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, September 1, 2013

LEO MWENGE CHRISTIAN CENTRE..

UJUMBE: BWANA ANAWATAFUTA WANA MAOMBEZI WAOMBEE KANISA.
MHUBIRI: Mch. Charles Kinyala
Maandiko: Ezekiel 22:23-31

Wakati ule Mungu Aliachilia nguvu za Roho Mtakatifu zitembee juu ya wana wa Israel lakini wana wa Israel wakamuacha Mungu wakaanza kuabudu miungu mingine, wakaruhusu vitu visivyo vya Mungu wa kweli, kwahiyo wakazuia Baraka na Nguvu za Mungu kufanya kazi juu yao. Na sisi kama kanisa inawezekana tumezuia mambo mazuri na kuruhusu mambo mabaya, tumezuia mambo ya kiMungu ndani yetu na kuruhusu mabo ya kishetani, maovu yetu yamemzuia Mungu kufanya kazi juu yetu kwasababu ya uovu wetu unatuweka mbali na Mungu. Sahivi watu wamemuacha Mungu, mpaka watu waliokuwa wanatumiwa na Mungu nao wamemuacha Mungu.

Leo zimezuka imani nyingi sana lakini sio zote ni za kweli, sio zote zinazo muabudu Mungu wa kweli, kwahiyo tunajifunza kwamba sio kila unabii ni wa kutoka kwa Mungu. Nabii nyingi sasa zinasema kuhusu mafanikio ya kimaisha yaani ya hapa duniani lakini hazisemi kuhusu maisha ya kiroho.

Shida nyingi zimetokea makanisani kwasababu makanisa sahivi yametoa uhuru mwingi, sisemi kwamba uhuru ni mbaya lakini uhuru unatakiwa uwe na mipaka, uhuru usio na mipaka ni mbaya!, watu wengi sasa wanavaa vibaya makanisani huku wakijitetea kwamba Mungu haangalii mwili anaangalia roho tu, huo ni uongo! huko ni kukosa hofu ya Mungu ndani yako.

Ikafika kipindi viongozi wa Israel wakashindwa kutofautisha mambo yaliyo ya ki-Mungu na yasiyo ya ki-Mungu, ni kwasababu ya kumuacha Mungu. Watu sasa wameshindwa kutofautisha mambo ya Mungu na yasiyo ya Mungu kwasababu Nguvu za Roho Mtakatifu zimeshaondoka mioyoni mwao hawana tena hofu ya Mungu ndani yao. Pia viongozi wa Israel wakawa wanawapa matumaini wakati pasipokuwa na tumaini, walikuwa wanasema mambo yao wenyewe alafu wanamsingizia Mungu kwamba ndio aliyesema na kumbe ni waongo.

Lakini Mungu anahitaji watu watakatifu, watu wanaomsikiliza na kuwa na hofu ndani mwao. Mungu anahitaji watu watakao mtumikia kwa roho na kweli, watu hao ndio waombee taifa letu la Tanzania, naye Mungu atasikia toka mbinguni

No comments:

Post a Comment