''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, September 8, 2013

UJUMBE WA LEO!!!UJUMBE: Heshima Yangu Kama Baba Iko Wapi Kwa Habari ya Zaka na Dhabihu?
MHUBIRI: Steven Wambura
MAANDIKO: Malaki 1:6-13

Sadaka imepoteza mvuto mbele za Mungu, imekuwa kitu cha kudharauliwa, watu hawaelewi tena maaana na uzito wa sadaka kabisa, watu wamekuwa wakitoa sadaka kwa mazoea. Wengi sasa wamekuwa hawatilii umakini kwa habari ya sadaka, zaka na dhabihu, hawamtolei Mungu sadaka za kumaanisha, kumbuka hakuna kitu cha bure bila kutoa sadaka utabakia hivyo hivyo,  Sadaka na sala za kornelio zilikuwa kumbusho mbele za Mungu (matendo 10:4), Mungu alizipokea sadaka za kornelio na kuzitakabali kwasababu alitoka sadaka ya thamani mbele za Mungu.

Kwanini sadaka sasa za watu wengi hazifanyi kazi?
Watu wengi sasa wamekuwa wakitoa sadaka bila kupata mafanikio kwasababu wanatoa sadaka zenye manung’uniko mbele za Mungu, walio wengi sasa wamekuwa wakitoa sadaka huku mioyoni mwao wana vinyongo, wamesema uongo, hawajasamehe wenzao, mioyo yao imejaa chuki na unafiki wakitegemea kwamba Mungu atapokea sadaka zao. Watu wanatoa sadaka wakati wamevunjika mioyo, wana manung'uniko mioyoni mwao.

Yawezekana umeomba sana bila kupata mafanikio na ukaanza kunung’unika lakini jiulize hivi leo je, umetoa nini kwa Mungu wako? Au yawezekana unatoa sadaka nzuri lakini kumbe hautoi fungu la kumi ndomana haubarikiwi, umekuwa mwizi kwa habari ya sadaka na fungu la kumi, na mambo yako hayafanikiwi na wewe kama binadamu unakuwa umechoka kuomba lakini kumbe shida ipo kwenye sadaka zako.

Leo makanisani watu wananung’unika na watu wanahoji na kuuliza wanataka kujua sadaka zinaenda wapi, hiyo inaonyesha kwamba wanamtolea mwanadamu na sio Mungu. Kitendo cha kunung'unika tu kwa habari ya sadaka yako laana inakupata pale pale, sadaka yenye thamani machoni pako ndio sadaka iliyo thamani machoni pa Mungu, kwanini utoe kilicho kinyonge ni mara kumi ukae usitoe kama siku hiyo huna sadaka ya thamani kwa Mungu.

Sadaka yenye thamani sio wingi wa pesa zako bali uthamani wa sadaka unategemea kile ulichonacho kwa wakati huo, anza na hicho ulichonacho kwa uaminifu. Unapoleta sadaka Mungu haangalii umebeba shilingi ngapi bali anaangalia nia yako unapokuja mbele za Mungu na sadaka hiyo. 

Sasa omba msamaha kwa kumaanisha ili Mungu aanze upya na wewe, amua leo kubadilika kama ulikuwa mwizi wa zaka badilika ili Mungu akubariki tena kwa Baraka za rohoni na za mwilini.

No comments:

Post a Comment