''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, September 15, 2013SOMO: NIDHAMU YA SADAKA
MHUBIRI: Mr. Steven Wambura
Maandiko: Mwanzo 22:2-3,Zaburi 50:5,15 

Ibrahimu aliambiwa na Mungu akatoe sadaka, na akamtolea Bwana kwa nidhamu. Swala sio kiasi gani cha pesa bali ni nidhamu ya kuitoa hiyo sadaka. Kuna maeneo matatu(3) ya kuzingatia kwa umakini wakati wa kutoa sadaka; nayo ni Eneo, Wakati na Aina ya sadaka. Ibrahimu aliambiwa aende mpaka nchi ya Moria(Eneo) akamtolee Mungu mtoto wake wa pekee Isaka(aina ya sadaka), Na Ibrahimu akatii agizo lile lwa nidhamu naye Mungu akambariki sana.

Unapotoa sadaka kuwa makini sana ya eneo la kuitoa hiyo sadaka, wakati wa kuitoa hiyo sadaka na aina ya sadaka utakayotakiwa kuitoa. Esau alikosa Baraka za urithi kwasababu hakuwa makini na muda. Inawezekana unatoa sana sadaka lakini haubarikiwi kwasababu hujawa na nidhamu ya muda wa kuitoa hiyo sadaka labda unawahi au unachelewa. Au inawezekana unatoa sadaka ya tofauti na uliyoambiwa, Mungu anakwambia utoe ng’ombe wewe unasema ngoja nitoe hela. Pia kuwa makini kwa habari ya muda, ukishasikia Roho Mtakatifu anakwambia peleka hela hii kwa mtu fulani, fanya hivyo muda ule ule panda hata bodaboda.

Kinacho kutoa katika matatizo ni sadaka na sio maombi, Musa alimuuliza Mungu kwamba nikienda misri nitamwambiaje mfalme wa misri akamwambia mwambie tunaenda kutoa sadaka kwasababu kitakacho kutoa kwenye matatizo yako ni sadaka, kitakacho kutoa misri ni sadaka yako, baraka zako zimefungwa katika sadaka katika Malaki amesema atafungua madirisha ya mbinguni na hakuna mahali pengine paliposema hivyo tena,  utafunga na kuomba sana lakini bila sadaka hutofanikiwa.
No comments:

Post a Comment