''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, September 29, 2013


UJUMBE: HABARI ZA UGEUKO WA BWANA YESU MLIMANI
MHUBIRI: Dr. Mumghamba
Maandiko: Marko 9:1-8, Mathayo 17:1-8,

Yesu alipanda mlimani na Petro, Yakobo na Yohana, gafla Utukufu wa Mungu ukashuka, Katika utukufu ule Musa na Elia walitokea pale. Bwana Yesu akageuka akawa na mng'ao wa ajabu, hayo ni mafunuo ya Bwana Yesu anavyotaka kujifunua kati kati yetu, Yesu ana njia nyingi za kujidhihirisha kati kati ya wanadamu.

   Petro akatoa wazo la kujenga vibanda vitatu cha Yesu, Musa na Elia lakini wazo hili halikutoka kwa Bwana kwa maana nyingine halikuwa sahihi. Yohana 14, inatuonyesha kuwa tunahitaji mafunuo ya Roho Mtakatifu ili tumjua Mungu tunaye mwabudu, kwamba Mungu habadiliki wala hapungui ndiye Yule Yule jana leo na hata milele. Ufunuo 1:9-12, Yohana alikuwepo katika roho ndomana akapata mafunuo yale, kwahiyo unapokuwa katika roho unapata mafunuo ya kutoka kwa Roho wa Bwana, ni jambo jema kuwepo muda wote kwenye uwepo wa Roho Mtakatifu. Petro alitoa wazo la vibanda lakini lilikuwa sio kutoka kwa Roho Mtakatifu, Mwambie Mungu aweke ulinzi katika kinywa chako ili maneno yako yawe yamekolea munyu ili yakamfae yule ambaye ni mhitaji.

  Neno likatoka kusema HUYU NI MWANANU MPENDWA MSIKILIZENI YEYE, tunatakiwa tumsikilize Yeye Bwana Yesu na sio mwingine, Ebrania 12:1-2, Unatakiwa umtazame Yeye peke yake(Bwana Yesu) na sio mwingine.Amen

No comments:

Post a Comment