''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, December 1, 2013

SIKU YA KUWASHUKURU WACHUNGAJI

UJUMBE: KAZI KUBWA ALIYOIFANYA BWANA
MHUBIRI: Mzee Kiongozi Dr. Mumghamba
Maandiko: Kutoka 14:10-15:3 

Mstari wa kusimamia ni wa 30, wana wa israel waliiona kazi kubwa Bwana aliyoifanya. Mwanzo walikuwa hawamwamini Musa kwamba atawavusha bahari ya shamu na wakaanza kunung'unika kwahiyo walikuwa wamekata tamaa, lakini baada ya kuona ile kazi kubwa Bwana aliyoifanya na ule wokovu mkubwa na kuona wale wamisri walivyokufa kwenye ile bahari wakaanza tena kumwamini musa. Kutoka 19:9, walikuwa wameondoa imani yao kwa musa kwahiyo Mungu ikabidi aingilie kati. Hesabu 14:9-12. 

Inawezekana Mungu anatenda matendo makuu kwako lakini hauyaoni. Watu kuzidi kuokolewa ni mambo ya Mungu hayo, tunapeleka injili vijijini watu wanatoka sehemu mbalimbali wanakuja kusikia neno la Mungu, na Yesu anawagusa wanaokoka hiyo ni kazi kubwa ya Mungu. 

Luka 9:28-36, macho yao waliuona utukufu wa Mungu, 2Petro 1:16-18, kutokana na shuhuda tulizonazo ni ushahidi kwamba Mungu anatenda mambo makuu kati yetu. Inatakiwa tuwaamini watumishi wa Mungu Tusiwaone kama wasanii bali tuwaamini. watu wengi siku hizi wamekuwa wana shida ya kuamini, wana mashaka na watumishi wa Mungu wanayoyasema, Marko 11:21-22, Tunatakiwa tumamini Mungu na sio kuwa na mashaka. 

Yeremia 1:11-12, alimuuliza Yeremia kwamba unaona nini? akasema naona ufito wa mlozi, na  Wana wa israel waliona kazi kubwa ya Mungu, je wewe unaona nini leo?. Upofu ukiingia unakuwa ni shida unakuwa huwezi kuona, ukiwa na upofu hauwezi kuona matendo makuu ya Mungu.  Ebrania 12:1-2, tumtazame Yesu Kristo, wewe unaona nini?, wenzetu wakaona utukufu wa Mungu katika ule mlima wa ugeuko, TUNAPASWA KUIONA ILE KAZI KUBWA ALUIYOFANYA MUNGU KWA WAISRAEL.No comments:

Post a Comment