''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, November 25, 2013

IBADA YA 28.11.2013

UJUMBE: UTUMISHI ULIO TUKUKA
MHUBIRI: Mzee Kiongozi Dr. Mumghamba
MAANDIKO: Kutoka 35:20-22, Kutoka 36:2-7, 2Wakorintho 8:1-5, Wafilipi 4:15-19  

Mungu alimuagiza musa kwa habari ya hema ya kukutania, na wale watu walileta vingi kwa wingi mno, na Mungu akaweka roho ndani yao ya kufanya vitu mbalimbali kama ni kuleta dhahabu na vingine vingi mpaka vikazidi sana, watu walileta vitu vingi mno mpaka Musa akasema tuwazuie wasilete tena, NI HABARI YA HIARI, UTUMISHI ULIO TUKUKA. 

Utayari wako mwenyewe kutoka ndani ni wa muhimu sana. Yesu alisema watu wakiacha kuimba mawe yataimba, utumishi kutoka moyoni. Watu wakatoa vitu vyao kwa moyo wa kupenda mpaka vikatosha na kuzidi na kuzidi. Moyo wa kumtolea Mungu kwa kumaanisha ndio unafanya huduma yako itukuke. Moyo wako uhimizwe kutoka ndani, ujihimize mwenyewe kutoka ndani sio mpaka uhimizwa, sio mpaka uambiwe toa sasa, 2Wakorintho 8:1-5, watu wa makedonia walikuwa masikini lakini walitoa kwa uwezo wao na zaidi ya uwezo wao na huo ndio utumishi ulio tukuka sio kwasababu wameshurutishwa bali ni kutoka kwenye mioyo yao.

Unapo toa kutoka ndani ndipo baraka za mbinguni zinapokujilia, Wafilipi 4:15-19, hizi zinatokana na moyo unaojihimiza kutoa ndani. Usukumwe wewe mwenyewe kumtolea Mungu ndipo utakapopata baraka kutoka mbinguni

 Kwasababu gani walisukumwa kutoka ndani? kwanini wengine wanasukumwa kutoka ndani na wengine hawasukumwi?, usiposukumwa na Neno la Mungu  hautapata msukumo, Roho Mtakatifu hawezi kukuongoza kama Neno la Mungu halijajaa ndani yenu. Treni ikitoka nje ya reli haiwezi kutembea mpaka urudi kwenye reli, toa kutoka ndani pasipo kusukumwa kutoka nje, wakatoa zaidi ya uwezo wao.

 Ukijawa na Neno la Mungu hutasukumwa kutoa, bali Roho Mtakatifu atatumia Neno kukwambia toa. Kwanini watu wa Makedonia wametushinda kwa habari ya kutoa, ni kwasababu walijazwa na  Neno la Mungu. Neno la Mungu likijaa ndani mwetu litatuongoza hata tutakuja wenyewe nyumbani mwa Mungu kuomba.  

Ziko baraka kwa watu wanaomtumikia Bwana kutoka ndani, Wafilipi 4:19, walitoa nafsi zao kwa bwana, usisubiri kulazimishwa, apandae haba atavuna haba, sadaka nzuri inatoka ndani na sio nje, wala haihesabiki kwa wingi wa pesa bali ulivyo maanisha kutoka moyoni. Uko uhusiano wa kile unachokitoa na uthamani wa Mungu ndani yako na hiyo ni ibada, jinsi unavyomthamini Mungu ndio ibada. Wengi tunafikiri ukitoa sadaka utakuwa masikini lakini hayo ni mahesabu kamili ya shetani, UTUMISHI ULIO TUKUKA UNASINDIKIZWA NA NENO LA MUNGU NDANI YAKO, KWAHIYO JAZA NENO LA MUNGU KWA WINGI MOYONI MWAKO KWA KULISOMA KWA WINGI.

Mzee kiongozi Dr. Mumghamba akiwa anahubiri ----------------------------------------------------------------------------------------------------------


Mrs. Kitwana akimshukuru Mungu kwa kupata shahada yake ya kwanza

Mrs. Kitwana akimshukuru Mungu kwa kupata shahada yake ya kwanza

Mzee wa kanisa Kitwana akimshukuru Mungu kwajili ya mafanikio ya mke wake

Dada Happy Mwaseba akimshukuru Mungu kwa kupata shahada ya pili (Masters Degree)
Dada Happy Mwaseba akimshukuru Mungu kwa kumpa shahada ya pili

Mrs Madauda akiwakilisha zawadi ya Happy Mwaseba kwa Mama Mchungaji
 --------------------------------------------------------------------------------------------

                            WATU WALIO TOKA MBELE KUMPA BWANA MAISHA YAO
 --------------------------------------------------------------------------------------------
                                                               
                                                                 SIFA NA KUABUDU..No comments:

Post a Comment