''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, February 23, 2014

USICHANGANYIKIWE MUNGU YUPO

MHUBIRI: Mch. Sanga
Maandiko: Kutoka 3:11-14, Kutoka 6:1-9

MIMI NIKO AMBAYE NIKO, Mungu yupo na ataendelea kuwepo. Mungu alijifunua kwa Musa ili akawaambie wana wa Israel kuwa atatimiza Neno lake na kwamba Yeye ni Yehova ambaye Ni Yehova anaye tenda alicho kiahidi, na kwamba ni  Mungu anayekumbuka agano lake.

 Tambua kuwa tunaye Mungu anayeweza kutenda alichoahidi, watu wanaweza kusahau, taifa linaweza kusahau lakini sio Mungu. Lile jeshi la farao lilileta hofu kwa wana wa Israel lakini Mungu akabakia kuwa Yehova. Musa alimuuliza Mungu nitajuaje kama Wewe umenituma, Mungu akamwambia nitakuwa pamoja na wewe. Haijalishi wewe unaumwa nini au unapitia katika hali gani Yesu yupo kwa ajili yako, Mungu ni mfalme wa wafalme, unaweza kujiuliza itakuwaje mshahara utakapo isha au pesa itakapo isha lakini tambua kuwa unaye Niko ambaye Niko unaye Mungu ambaye yuko alikuwepo na ataendelea kuwepo. 

Jina la Mungu lina uwezo mkubwa, Mungu anaweza kubadilisha historia yako sio kwa jitihada zetu au za matabibu lakini kufumba na kufumbua Mungu anaweza kubalisha maisha yako, acha kujiuliza itakuwaje wewe muachie Mungu. Yesu ndiye Jibu, Musa akauliza maswali mengi ya je ikiwa.., je ikiwa waisraeli wasipo nisikia itakuwaje?, je ikiwa farao akanifukuza itakuwaje?. inawezekana na wewe unajiuliza je ikiwa mtihani usipo faulu.. lakini kumbuka kwamba upo msaada utokao juu, ni kweli shetani atakupa maswali ya hivyo lakini usichanganyikiwe Yesu yupo pamoja nawe/nasi, Usichanganyikiwe Yesu yupo!

MAMBO YANAYOFANYA WATU KUCHANGANYIKIWA 

1.Hali ya kuwaza na kuwazua, Ayubu alivyo jaribiwa hakumuwazia Mungu vibaya.
2.Hali ya kujaribu kutatua kila kitu kwa kutumia uwezo,akili ulizo nazo, kuna mambo ufahamu wako kama mwanadamu utakataa, akili itakataa lakini Mungu yupo anayeweza yote.
3.Kutokufuata Mungu na Njia zake, Musa mtumishi wa Bwana alijua njia za Bwana, na yawezekana Musa alijujaje njia za Mungu, ni kwasababu kila alipopata shida alienda mbele za Mungu na kusikiliza kile anachotaka ufanye. Kuwa na tabia na hali ya kupenda kumtafuta Bwana. 
4.Kuacha kumwamini Mungu, kuacha kuwa na Imani, anasema mtumishi wake ataishi kwa imani naye akisitasita roho yake haina amaninaye. 
5.Hali ya kutomshirikisha Mungu kitu unachikiona, wengine wakisikia kitu wanachanganyikiwa, ni kweli unasikia mengi lakini je Mungu anasemaje?, Elia alifanyia kazi maneno ya yezebeli kwamba atauwawa akakimbia. Mungu alichokisema kina uhakika, mwenye haki wangu ataishi kwa imani. 

Usichanganyikiwe tunaye Mungu mwenye uwezo wote Mathayo 14:22. Hicho unachokiona haimaanishi kuwa Yesu hayupo hata kama unapitia katika shida ya ngumu kiasi gani lakini Yesu bado yupo, lazima umjue Mungu uliye naye, anakumbuka alichosema juu yako.Yesu yupo.

No comments:

Post a Comment