''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, March 9, 2014

KARIBU MWENGE TAG

UJUMBE: KUTII KUNAKOWEZA KULETA MAJIBU YA SHIDA YAKO. 
MHUBIRI: Mch. Grace Mainoya. 
Maandiko: 2Wafalme 5:1-16, Mathayo 28:28

Kutii ni muhimu sana, katika maandiko ya myuma kidogo tunaona jinsi mfalme sauli mfalme wa kwanza wa israel hakutii sauti ya Mungu ya kwamba aangamize kila kitu lakini hakuangamiza kila kitu kama alivyo ambiwa na madhara yake akanyang'anywa ufalme akapewa Daudi. Na mfano mwingine ni Tairo alimfwata Yesu akamwambia mtoto wake anaumwa sana baada ya muda kidogo Tairo akaambiwa na mtumishi wake kwamba binti yako ameshakufa, lakini Yesu akamwambia Tairo amini tu mtoto atapona na tairo akatii na akaamua kuamini hivyo na Yesu akamfufua binti yule. 

2wafalme 5:1-16, Naamani alikuwa jemedari wa vita lakini alikuwa na shida moja alikuwa na shida ya ukoma , unaweza kuwa na magari mengi au pesa nyingi lakini kumbe una shida kubwa ambayo hakuna mtu anaye weza kukusaidia , lakini Yesu kristo tu ndio mwenye uwezo wa kukusaidia shida yako. Naamani alifikiri yale maji ndio yatakayomponya, sijui shida yako lakini usikate tamaa wengine wanakata tamaa wakati ndio jibu limefika kabisa alafu ndo wanakata tamaa, Naamani alijichovya mara ya kwanza mara  ya pili na ya tatu mpk ya saba na ngozi yake ikawa nzuri kama ya mtoto.

 Ebrania 10:35-, Ukiamua kuamini amini na usikate tamaa, inawezekana umeomba sana lakini usikate tamaa, kumbuka mto yordani kulitokea miujiza sana,  Elia alipiga maji ya mto ule na koti lake maji yakagawanyika na elisha alipokuwa anarudi akafanya hivyo hivyo. Mungu anaweza kutumia kitu chochote kutenda muujiza kukuponya wewe mathayo 28:28, je ni mzigo gani ulionao? je ni shida gani uliyonayo?, Yesu leo yupo kwa ajili yako, je una shida gani iyayokufanya hata usipate usingizi?, mwambie Yesu shida yako, amini tu yote yanawezekana. na uponyaji wetu ni bure ulilipiwa na damu ya Yesu.naamani aliona utukufu wa Mungu, zilete shida zako kwa Yesu, isaya 58:1-, mawazo ya Mungu ni ya tofauli sana si kama mawazo yetu, pia wengi hawatii ndomana hawabarikiwi kwasababu hawatii.  Lakini tuache dhambi, dhambi inatufanya tuwe mbali na Mungu

No comments:

Post a Comment