''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, April 13, 2014

JIWEKE WAKFU KWA BWANA..

Mhubiri: Mchungaji Kiongozi Mhini
Maandiko: Yohana 17:13-26

Yohana 17:13-26, 
 Haya ni maombi ya Yesu aliyowaombea wanafunzi wake na watakao okoka huko mbele. Haya ni maombi ya kujiweka wakfu kwa Bwana, aliyaomba ili kujitenga kwa kazi maalumu ya kwenda msalabani, na Bwana Yesu akijua saa yake ishafika alitumia saa hiyo kujiweka wakfu kwa Bwana na alijua anaondoka lakini kuna watu atawaacha kwahiyo akawakabidhi kwa Baba yake wa Mbinguni.

 Sisi tuna uraia wa muda mfupi wa hapa duniani lakini tuna wa kudumu wa Mbinguni, tunaingia katika kipindi cha mateso ya Yesu Kristo huku tukijua kwamba kwa kupitia mateso ya Yesu wokuvu tumeupata.

Katika mstari wa 15. Yesu aliomba watakao baki waliepushwe na yule mwovu, usumbufu wa ibilisi katika maisha yetu upo na Yesu alitambua hilo. Dunia sio mahali pako, usijichanganye na dunia, fanya kama Mfalme wako anavyotaka yaani Yesu kristo, kaa umuishie Mungu na ulinzi wake utauona, Yesu alisema hawa sio wa ulimwengu. Sasa Umewekwa wakfu ili Bwana Yesu akutumie tunapeleka injili ili tutumike kwa ajili ya Bwana. Sasa kinachotakasa ni ile kweli ambayo hiyo kweli ni Yesu mwenyewe. Usibwete na kukosa amani tunaye Yesu Kristo anayetuombea kwa Bwana, tuwe na umoja tukisema tufanye hivi katika umoja ule ule tunafanya tukisema maombi basi wote tuombe, ndomana anasema wote wawe na umoja kama Wao walivyokuwa na umoja, tuyafanye mambo yetu tukiwa ndani ya Yesu Kristo na sio nje ya Yesu. Pia alisema utukufu ulionipa nawapa wao alitutukuza, kupitia Yesu Kristo tukamjua Baba. 

NIA au KUSUDI LA BWANA YESU  KWAKO.
1. Utende mapenzi ya Baba yake yaani Mungu 
2. Uwe kielelezo kwa wanafunzi ili nao waweze kutengwa na dunia 
3. Uwe tayari kutengwa kwa kazi maalumu. Yesu alionyesha kuwa tayari kwa kazi maalum ya ukombozi, Je una utayari wa kiasi gani kufanya kazi ya Mungu? Usiwe mtu wa kukimbia na kuogopa, Warumi 6:1-2, 8:8-, 17:17, katika maombi yako nenda na kanuni za Mungu na sio zako, unapo muomba Mungu usiombe tu bali Imani iwe ndani, Wakolosai 4:2, 
4. Upende haki na kuchukia uovu, watu wa mataifa sio wapenda haki lakini wewe mtu wa Mungu penda kufanya haki usipende dhuluma ebrania 1:9, 
5. Udumu katika ujazo wa Roho Mtakatifu, jiulize kwanini umekaukiwa na Roho Mtakatifu Warumi 8:14, Ongozwa na Roho wa Mungu, Roho wa Mungu akupe mwelekeo/ direction. Ukizingatia haya utaona utofauti na endelea kujiweka wakfu, na uyafanye mapenzi ya Kristo.

2 comments: