''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, June 1, 2014

SIKUKUU YA WATOTO

UJUMBE: UTII
Mhubiri: Mary Emili
Maandiko: Waefeso 6:1-9, Wakolosai 3:18-22

Unapotii unapata baraka nyingi kutoka kwa Mungu. Kuna aina nyingi za kutii, 1.kuwatii wazazi, 2.kuwatii mabwana zetu.
Unapotii wazazi unapata miaka mingi ya kukaa au kuishii  hapa duniani. Unaweza kujiuliza kwanini kuwatii wazazi?  kwasababu ni amri kutoka kwa Mungu yenye ahadi kumbukumbu 6:24

Pia kwasababu ukiwatii Mungu ameahidi kutubariki kumbariki mtu anayetii wazazi wake kumb 5:16, unapotii wazazi unapata baraka kutoka kwa Mungu, hasara ya kuacha kuwatii wazazi ni kunapelekea kuvunja amri nyingine kama mzazi akisema usiibe usipotii utaenda kuiba na utakuwa umevunja amri ya kutokuiba. Pia utapata miaka michache yenye hasara,

2. Kuwatii mabwana zetu, kama wewe ni mfanyakazi unatakiwa uwatii mabosi wako yawezekana wanakwaza sana lakini unatakiwa uwatii hata kama wananyanyasa, unatakiwa ujitaidi kuwatii  si kwa jinsi ya mwili au hofu bali kwa kumtii Kristo. Lakini pia mabwana wawape watumwa wao haki yao sio kwaajili yetu ni kwa ajili ya utukufu wa Bwana Yesu, wape  wafanya kazi wako haki zao mkijua kuwa na ninyi mna Bwana wenu mbinguni, wakolosai 4:1. Kama umemuajili mtu hata dada wa nyumbani usiwanyanyase, na hata kama umeajili wafanya kazi ofisini wape posho zao kwa muda unaotakiwa

Jinsi utii unavyoweza kuleta mafanikio 

Ukitii Neno la Mungu utapata mafanikio, Mungu anaweza kutumia watumishi wake kukuletea ujumbe, ukitii utapata faida lakini usipo tii utapata hasara kubwa sana, kwa mfano Mfalme Sauli aliambiwa akaangamize waamaleki wote na kila kitu chao, yeye akafanya kama alivyoona yeye na hakuwaangamiza wote akamuacha mfalme wa amaleki Bwana akamuondolea Ufalme kwa kosa hilo tu. Kosa lake lilikuwa kufanya alivyoona yeye, Je wewe huwa unatii? Au unafanya kama unavyoona wewe?

Miss Mary Emili

No comments:

Post a Comment