''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, July 27, 2014

MAUMIVU YA KAKA JUU YAKO

Mhubiri: Mch. Peter Mitimingi
Maandiko: Luka 15:20-32

kaka ni ndugu, kaka ni mtu wa karibu, kaka ni mtu ambaye unategemea afurahie mafanikio yako, afurahe unavyoenda mbele lakini inakuwa vibaya pale kaka badala ya kufurahia  maendeleo anaumia, kaka anaumia kwanini umefanikiwa, kaka anatamani kuona kwamba umeishiwa. Luka 15:15-20,20-32, inazungumziwa kuhusu habari ya mwa mpotevu, mwana mpotevu aliomba urithi wake, baada ya kupewa urithi wake alienda  nchi ya mali ktapanya mali zake kwa anasa mpaka akaishiwa. Alipoishiwa akakumbuka nyumbani kwa baba yake. Hapa tunapata picha mbili, moja tunamuona baba wa mwanampotevu ambaye katika somo hili ninamfananisha na Baba Mungu.

Baba wa mwana mpotevu anamuwazia nini mtoto wake aliporudi, Baba Mungu wa Mbinguni anakuwazia nini wewe mwana wake. Na picha ya pili ni kaka wa mwana mpotefu, kaka wa mwanampotevu alimuwazia nini mdogo wake aliporudi nyumbani?

Mtazamo wa baba juu ya mwana ni nini?
  1. Baba alimuona mwana tokea mbali, yawezekana pale kulikuwa na wafanya kazi wengi lakini hawakuona kuwa yule ni mtoto wa nyumbani kwao, macho ya baba yalimuona tokea mbali. Macho ya Mungu yanakuona tokea mbali, Mungu anakuona 
  2. Baba alimuone huruma akampoke kwa furaha


---------------------------------------------------------------------------------------------------
IBADA YA JIONI YA KUSIFU NA KUABUDU



Picha ya pamoja baada ya ibada

No comments:

Post a Comment