''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, September 21, 2014

NJOONI WOTE MSUMBUKAO

Mhubiri: Mchungaji Sanga
Maandiko: MATHAYO 11:25-30

Maneno haya aliyazungumza Yesu na aliyasema kwa ajili yako/yetu ya kwamba anamshukuru Mungu wa mbinguni kwa kuwafunulia watoto wachanga kumjua Yesu ni nani, pia akasema nimekabidhiwa YOTE na Baba yangu, na yoyote Baba anayopenda humfunulia, akasema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo. Mara nyingi ikiongelewa habari ya mizigo wengi wanajua ni mizigo ile ya watu wasioamini wasiookoka, lakini unaweza kuwa umeokoka lakini bado umebeba mizigo moyoni mwako, umebeba chuki, umebeba hasira, umebeba kuto salimiana na mpendwa mwenzako, umebeba machungu kwa ajili ya watoto, umebeba machungu kwa ajili ya kazini lakini Yesu anasema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha, Haleluya!. Yesu ana uwezo wa kupumzisha maisha yako, tabu unayopitia, shida unayopitia yuko mbeba mizigo Yesu Kristo, hustahili kubeba wewe Yesu anaweza kubeba maisha yako, anaweza kubeba magonjwa yako, Yeye ndiye Mungu, anasema njooni wenye kulemewa na mizigo naye atawapumzisha. Sikia, Mungu aliye tuokoka ndiye anayejua njia ya mwanadamu mapito ya mwanadamu, njia wanadamu wanazopitia ziko mikononi mwa Mungu, Yeye aliyeziumba Mbingu na nchi kwa fahamu zake anasema njooni msumbukao na Yeye atakupumzisha. 

Yesu atakupa raha kazini kwako, nyumbani kwako, Yesu anaweza kuleta raha kwako hakuna mwingine anayeweza kuleta raha y6a kweli kama Yesu. Tatizo linakuja hapa, unaacha kumpa Yesu mzigo wako, unaacha kumpelekea Yesu shida zako, wakati mwingine huelewi mahali sahihi pa kupeleka, nakwambia peleka kwa Yesu, mwambie shida hii naileta kwako, ugonjwa huu nauleta kwako na Yesu yuko tayari kukusaidia. Yesu ana uwezo wa kushughuka na matatizo yako.

No comments:

Post a Comment