''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, October 19, 2014

UTOAJI WA MUNGU NA UTUNZAJI WAKE NI WA AJABU

Mhubiri: Mch. Grace Mainoya
Maandiko: 1Wafalme 17:8-24, Mathayo:10:40-42

Hapa tumesoma habari za nabii Elia na mjane wa sarepta, Nabii Elia ni nabii aliye jaa nguvu za Mungu na mwenye imani kubwa hata akafunga mvua kwa miaka mitatu na nusu isinyeshe mpaka alipo omba tena badae ndio mvua ikanyesha. Na kwanini alifungua mvua, ukianza kusoma kwanzia mlango wa 16, Israel walimuacha Mungu wa kweli aliye waokoa katika nchi ya utumwa, aliye wavusha bahari ya shamu, aliyewapa mana jangwani, aliyeuangusha ukuta wa yeriko, aliye warithisha kaanani yenye maziwa na asali aliyowaahidi na kuanza kuabudu baali, walianza kuabudu baali kwasababu Mfalme Ahabu aliona mwanamke wa sidoni aitwae yezebeli aliyekuwa anaabudu mabaali, na miungu hiyo akaja nayo Israel na akamjengea madhabahu mungu baali, baada ya hapo ibada Israel ikabadilika badala ya kumwabudu Mungu wa Kweli wakaanza kuabudu mungu baali. Ndipo Nabii Elia akainuliwa na Mungu, akasema hakutakuwa na umande wala mvua mpaka kwa neno lake ili ijulikane Mungu wa Israel ndio Mungu na anapaswa kuabuduwa Yeye tu.

Mungu kwa ulinzi wake na utunzaji wake alimwambia Nabii Elia aende karibia na kijito cha Kerithi na huko akawa analishwa na kunguru mkate na nyama asubuhi na jioni na kunywa katika kijito kile, Haijalishi unapita katika hali gani au upo kwenye shida gani Mungu anaweza ainue kitu chochote kikusaidie kwa wakati huo kama alivyomtumia kunguru cha muhimu endelea kumtegemea Mungu. Lakini Mungu hakuishia hapo tu baada ya kijito kile kukauka neno likamjia tena Nabii Elia kwamba aende Sarepta huko kuna mwanamke mjane Mungu aliye muweka ili amlishe, Mungu aliendelea kumlinda Nabii Elia na kumuokoa na mkono wa yezebeli.

No comments:

Post a Comment