''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, November 16, 2014

NAFASI YAKO KATIKA KUMJUA MUNGU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Mhini
Maandiko: Yohana 17:1-19 

Yesu alijua mateso atakayoyapata na akaamua aombe maombi hayo, tunamhubiri Yesu kristo mwenye mamlaka mwenye nguvu isiyoweza kuzuilika na kitu chochote. kuokoka ni hatua moja lakini ya pili ni kumjua Yesu, unayo nafasi ya kumjua Mungu.

MAMBO YA MSINGI
1. kwanini Mungu Yupo?
2. Mapenzi ya Mungu ni nini? au Mungu anataka nini kwangu?
3. Je unamjua Mungu au unampapasa? Hesabu 6:22, 
4. Lazima uwajulishe wengine wamjue Mungu
5. Je unafanya juhudi gani ili wengine wamjue Mungu?

Zingatia Mambo Yafuatao 
1. Hakikisha umetengwa na watu wa dunia hii, lazima watu wa dunia hii watambue kwamba umetengwa na dunia hii. Mathayo 10:34-39 
2.Huduma ya unyenyekevu na kubeba msalaba lazima uizingatie 
3. Jikane mwenyewe kwa ajili ya Kristo 
4. Imani yako lazima ithihirike kwenye vitendo

No comments:

Post a Comment