''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, December 21, 2014

WEWE NI MWANA WA MUNGU

Mhubiri: Mr. Emmanueli Mahundo
Maandiko: Luka 15:11-32 


Fahamu kuwa Mungu alivyokuokoa alikuhamisha kutoka utawala  wa shetani akakuingiza katika utawala wa mwana wa pendo lake, lakini baada ya kukuhamisha akakuacha hapa duniani  kama watoto wake.  Kwahiyo kama umeokoka,  hivyo jinsi ulivyo ni mtoto wa Mungu.  Yohana 1:12-13 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.  Wewe ni motto wa Mungu na kuzaliwa kwako si kwa mapenzi ya mwili bali umezaliwa kwa mapenzi ya Mungu.
Mungu amekuacha wewe mtoto wake hapa duniani ili watu wengine wakitaka kumjua wakuone wewe waone jinsi unavyoishi jinsi unavyoenenda. Kimwili tunategemea mtoto awe anafanana vitu flani na baba yake, sasa Yesu alipokuokoa anategemea uishi maisha matakatifu kama Baba yako Mungu alivyokuwa mtakatifu. Neema ya Mungu inakuwezesha wewe mwana wa Mungu kuishi maisha ya kukataa uovu katika dunia ya sasa.
Wewe ni mtoto wa Mungu na ndomana Mungu ameweka mamlaka ndani mwako na Mungu anakupenda hivyo jinsi ulivyo.

No comments:

Post a Comment