''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Thursday, January 1, 2015

FANYA TATHIMINI, WEKA MALENGO MAPYA NA UYATEKELEZE

Mhubiri: Mchungaji Kiongozi Mhini
Maandiko: Wafilipi 3:12-16

Mtazamo wa Paulo katika maisha yake ya kirumu ilikuwa hajizanii kama amikwisha kufika, pamoja na safari zake zote pamoja majaribu yote aliyopata lakini anasema hajizanii kama amekwisha kufika. Alikuwa analiambia kanisa la Filipi, kanisa hili lilikuwa na moyo wa utoaji, moya wa umisheni na kupeleka injili, hawakujali umasikini wao hawakujali ufukara wao lakini walizidi kutoa kwa ajili ya injili, mara nyingine mtu huwezakusema mimi nitatoaje hela zenyewe hizi ndogo, lakini kanisa hili hawakujali kidigo walicho nacho lakini walitoa kwa ajili ya Bwana.
 
Paulo aliendelea kusema anakaza mwendo, mtu akisema anakaza mwendo inaonyesha ndani yake ana nia ya kusonga mbele, Je wewe umeridhika na hapo ulipo? Je umeridhika na mambo uliyofanya mwaka 2014? kwamba umesha kwisha kufika kwahiyo hakuna haja na hatua zaidi? lakini Paulo alisema hajakwisha kufika lakini huyu ndiye aliyeandika vitabu 13 wingi kuliko mitume wote lakini pamoja na elimu kubwa aliyonayo alisema hajizanii kama amekwisha kufika, bado nina kaza mwendo. sasa na wewe usijizanie kama umefika lazima ujue ni kasi gani utakayo ondoka nayo na ukase mwendo kiasi gani, hata kama kuna majaribu mengi lakini kaza mwendo. Kaza mwendo kwenye kupeleka injili, toa kwa ajili ya injili lakini pia hebu jiulize mwaka 2014 ni wangapi umewaleta kwa Yesu? na hao ulio waleta kwa Yesu je umefuatilia ni wangapi mpaka leo wamesimama vizuri na wanaendelea kula nyumbani mwa Bwana?.
 
Inawezekana kabisa mwaka 2014 hujamshuhudia hata mtu mmoja unajali tu ya kwako, Mungu amekuokoa ili uwalete wengine kwa Yesu, neon hili ni kubwa sana, ndio utaimba utaruka ruka lakini siku ikifika Bwana Yesu atakuuliza uliwaleta wangapi kwa Yesu?. Pia changia injili, unaweza kupangilia vitu vingi na sadaka kidogo lakini tambua kuwa pesa sio yako hata kama zipo nyingi benki, yupo aliye kuwezesha uzipate, sasa huyo aliyokuwezesha huyo ndio anastahili kuwa nafasi ya kwanza.
 
Uguse moyo wa Mungu kwa kutoa kwa ajili ya umisheni, kwa kutoa kwa ajili ya injili na utabarikiwa sana. Pia kama Paulo anavyosema, sahau yaliyoko nyuma na chuchumilia yaliyo mbele, sahau yaliyo tokea mwaka 2014 na anza upya na Bwana na kaza mwendo. Chuchumilia yaliyoko mbele yako kama umejiwekea malengo katika mwaka huu mpya basi chuchumilia hayo, timiza yale malengo uliyo jiwekea unaweza kusema mimi mwaka huu nitatoa kiasi hiki kwa ajili ya injili na timiza, Hakuna Baraka zisizo na gharama lazima kuna gharama katika Baraka kama Mungu akikubariki gari hili gari ujue lina gharama ya kuweka mafuta, kufanyima service. Hakuna Baraka zisizo na gharama, wokovu ulionao una gharama na gharama yake ni kwenda kuwaleta wengine kwa Yesu maana Bwana Yesu amekuokoa kwa ajili hiyo. Fanya tathimini ya mwaka jana uliyatekeleza vipi na kiasi gani, alafu weka malengo mapya na uyatekeleze. Pia usiwe na tabia ya kuridhika na kuacha kuchuchumilia yaliyo mbele, Kuridhika ni sumu ya maendeleo.

 

No comments:

Post a Comment