''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, January 17, 2016

MUNGU ANALIITA KANISA LA KARNE YA 21 LIRUDI KATIKA MIZIZI YA UMISHENI

Mhubiri: Samwel Nshasi
Maandiko: Yohana 20:21, Matendo 1:8, 13:2-3,


 Yesu alikuwa anawaambia wanafunzi wake, Yeye alitumwa kulileta kusidi la Mungu la kuokoa mwanadamu lakini sasa muda umefika ambao ninawapa ninyi mamlaka yote, na sisi leo ndio wanafunzi wa Yesu Kwahiyo Yesu alitupa jukumu moja kubwa la kupeleka injili na mamlaka yote ametupa. Mamlaka ya Jina la Yesu ndio inayotuwezesha leo kuwaambia watu habari njema za Yesu na wakaokoka sio hilo tu bali pia ndiyo inayotuwezesha kutiisha nguvu zote za mwovu shetani.
 
Yesu alipoondoka alituachia kanisa mamlaka kwa maneno mengine Kanisa ina mamlaka ya Yesu Kristo, Kwahiyo kanisa lina mamlaka katika ulimwengu, kanisa lina majibu katika ulimwengu. Kanisa ni chombo pekee ambacho hakiwezi kushindwa kutoa majibu ya ulimwengu, kutoa majibu ya wanadamu kwasababu lina mamlaka ya Mungu.
 
Kanisa lilipita katika vipindi mbalimbali katika karne tofauti tafauti lakini sasa Mungu anaasa kanisa la karne ya 21 kwamba turudi katika mizizi ya umisheni. Umisheni ndio kazi aliyotuachia Mungu na ndio iliyoujaza moyo wa Mungu sana. Wewe kama mmoja wapo wa kanisa Mungu anakukumbusha jukumu lako, Mungu anakukumbusha kwamba unatakiwa kutangaza Neno la Mungu katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Jitaidi wewe kama mtumishi wa Mungu shuhudia kwa bidii, usipande na mtu kwenye basi kwenda safari ndefu bila kumshuhudia, ni hasara kubwa sana mtu akifia katika dhambi yake na hilo lamsikitisha Mungu sana.

No comments:

Post a Comment