''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, January 31, 2016

MPANGO WA MUNGU WA UKOMBOZI

Mhubiri: Mch. Elias Mussa
Maandiko: Kutoka 3:1-8,14-15, Yohana 4:7
 
Mpango wa Mungu wa ukombozi, unaangalia dunia iliyoanguka na jinsi Mungu anapotoka kuirejesha au kujifunua katikati ya wanadamu. Kutoka katika kitabu cha mwanzo tunaona kuwa Mungu huwa anatafuta mtu katika bustani ya edeni, Mungu alimtafuta mtu ili kumuonyesha mwanadamu kuwa unawajibika kwa kile unachofanya. Usipotaka kuwajibika Mungu huwa anakupa hukumu.

Nuhu alihubiri zaidi ya miaka mia moja ili amuokoe mwanadamu lakini watu wale hawakuokoka kwasababu ya ukaidi wao; pia kipindi cha Ibrahimu, uzao wake ukaenda utumwani miaka mia nne lakini baadae Mungu akatafuta mtu wa kuwaokoa watu wale kutoka utumwani, shetani alipojua kuwa kuna mkakati wa kuwakomboa watu wale alitaka kuharibu mpango lakini Mungu alimsaidia mwanadamu na mpango wake haukuharibika.
 
Tunaposema mpango wa Mungu wa ukombozi ina maana ya kuwa Mungu ana mpango kamili wa ukombozi lakini anatafuta MTU wa kuimalizia ile kazi.
 
KUNA MAMBO MAWILI YA MPANGO WA MUNGU WA UKOMBOZI
        1.Ujumbe wa Ukombozi

        2.Mjumbe wa Ukombozi

KUTOKA 3:1-6
Hapa tunaona Mungu amempata mtu wa kufanya kazi yake ambaye ni Mussa. Mungu akaweka kitu cha tofauti ndani ya Mussa ili asije kwenda nje ya lengo na badala yake apende kuwa karibu na mpango wa Mungu.
Kutoka hapa tunajifunza mambo haya;-

1.Mtu anayeitwa na Mungu lazima akutane na Mungu mwenyewe-Katika Matendo 9:.. Paulo alikutana na Mungu na kupewa maagizo kuhusu mpango wa Mungu.
-Katika Yohana 4:.. Mwanamke kutoka samalia alikutana na Mungu ndipo naye akaujua mpango wa Mungu.

*ili uweze kushuhudia mpango wa Mungu lazima ukutane kwanza na Mungu na ndio upate kujua mpango wa Mungu na hapo ndipo ambapo utaweza kushuhudia. (LAZIMA UKUTANE NA BWANA)
 
2.Lazima uwe na uwezo wa kuisikia sauti ya Bwana na kuitii
Kutoka 3:7-8, Kama masikio yako ya rohoni yameziba hata kama mtu atahubiri na sifa za aina zote za Mungu itakuwa ni kelele tu katika masikio yako.

Yohana 4:7-.. Yule mwanamke msamaria alimsikia Yesu.
 
3.Lazima tuwe Na Ufahamu wa Jina la Mungu AliyetutumaKutoka 3:14-15, Kama hujui jina la aliye kutuma huwezi kufanya kazi yake sawasawa maana utashindwa kujieleza.
 
4.Hakikisha una Uweza, Nguvu na Mamlaka.Hata Musa alipewa kwanza uweza, nguvu na mamlaka ndipo akaenda kuanza kutekeleza mpango wa Mungu.
"Usipange kushuhudia kama hujapata nguvu na uweza na mamlaka ya kutekeleza mpango wa Mungu."
 

No comments:

Post a Comment