''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, April 10, 2016

KUSIKIA SAUTI YA MUNGU

Mhubiri:Mr. Frank Mwalongo Maandiko:Luka 4:1-4

Sisi kama watoto wa Mungu kusikia sauti ya Mungu ni lazima na hii sio kwa ajili ya mchungaji lakini kila aliyeamini na kumpa Bwana Yesu maisha yake. Kitabu cha zaburi kinaelezea jinsi wana wa Israeli walivyosafiri kwenda kaanani kwa muda mrefu wakati ilikuwa ni safari fupi. Ilikuwa hivyo ni kwa sababu hawakusikia sauti ya Mungu. Kama watoto wa Mungu kila mmoja wetu anapaswa kutambua sauti ya Mungu wetu Yesu Kristo.

Mungu wetu anaongea na yeyote yule aliye mwaminii. Kila mtu aliye okoka inapaswa aweze kuisikia sauti ya Bwana Yesu. Wakati tunaishi maisha yetu leo tukumbuke kwamba tunatakiwa kutia bidii katika kuisikia sauti ya Mungu, kama hatutatia bidii kuisikia sauti ya Mungu basi Mungu hatazungumza nasi pia. Ili usikie sauti ya Mungu lazika uombe kwa bidii sana na usipoisikia unaendelea kuomba mpaka uisikie sauti yake. Hiyo ndiyo bidii ya kuisikia sauti ya Mungu

Mungu ana wakati wake wa kusema nasi kwa hiyo tunatakiwa kuendelea kuomba hadi wakati wa Mungu ufikapo wa kusema nasi,na atasema nasi. "TUENDELEE KUOMBA,TUMWAMBIE MUNGU TUNATAKA KUSIKIA SAUTI YAKO,TUNATAKA KUSIKIA UKISEMA NASI"

No comments:

Post a Comment