''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, April 18, 2016

MUNGU NDIYE MPAJI WA KILA KITU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Meshark A. Mhini
Maandiko: Yohana 6:1-15

Yesu ndiye mpaji wa mahitaji yetu, fahamu kuwa Mungu ndiye mpaji wa kila hitaji lako. Muda mwingine unajisahau na kuona kama kila kitu kinachoendelea ni kawaida lakini Mungu ndio mpaji wako wa kila kitu. Mungu yuko makini sana sana kuhakikisha kwamba unapata kila hitaji lako ulilo muomba. Yohana 6:1-15, umeona Mungu mpaji, watu elfu tano ukiacha wanawake na watoto walikuwa na kusaza kutoka kwenye mikate mitano na samaki wawili.

Muda wote kuwepo katika mapenzi ya Mungu, ukiwa mwaminifu kuomba na kusoma Neno na kuwa mtakatifu Mungu atakuwa mwaminifu kukupatia mahitaji yako yote. Sisi kama binadamu tuna mahitaji tofauti tofauti na muda mwingine unapitia majaribu lakini ukiwa karibu na Mungu, Mungu yupo tayari kukupatia unachohitaji, inawezekana unaumwa Mungu ndiye mponyaji wa ajabu anayeweza kukuponya chochote hata wanavyovishindwa matatibu wa hapa duniani.

Usikate tamaa unapoona umeomba na bado hakijatokea endelea kuomba na kuomba mpaka upate jibu. Katika mstari wa 5, wanafunzi wanamuuliza Yesu kwa kumjaribu kuona atafanyaje lakini Yesu anakuwa tayari ameshapata jibu la hitaji lako kabla hujaomba anacho subiri ni wewe kuomba na kusema nini unacho hitaji, Zaburi 111:5-6, kwahiyo ukinyenyekea Mbele za Mungu, Mungu atakusikia kwasababu ni Mungu wa maagano na atatuma malaika wake aje kukusaidia, inahitaji uwe mnyenyekevu. Zaburi 104:23, Wafilip 4:14-16. Mungu ana uwezo wa kukuponya kiroho na kimwili. Hata kama ukipita katika majaribu magumu sana kumbuka kwamba uko pamoja na Yesu, na unapoomba omba kwa imani. Omba na utapewa.

No comments:

Post a Comment