''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, May 1, 2016

AINA 3 ZA WATOAJI

Mhubiri: Dkt.Mch. Peter Mitimingi
Maandiko:
Mathayo 25:24-27

Kulikuwa na tajiri mmoja alikuwa akifanya biashara za madini, sasa njiani kuelekea kule mgodini kulikuwa na masikini aliyekuwa akiomba omba kwa siku nyingi, lakini tajiri yule kwa siku nyingi tu alikuwa akimpita bila kumsaidia ,siku tajiri yule alivyokaribia kupata madini aliadhimia kwamba akipata madini atamfanyia kitu kikubwa sana yule masikini ambacho kitabadilisha kabisa maisha yake na sio kumpa pesa ndogo tu, siku akapata madini mengi akaenda kwa yule masikini akamkuta anakula korosho, yule tajiri akasema moyoni mwake kwamba atamuomba korosho yule masikini na idadi za korosho atakazo mpatia idadi hiyo hiyo atampa dhahabu lakini cha kushangaza yule masikini akamnyima kabisa tajiri zile korosho na kuanza kusema wewe ni tajiri mkubwa sana una mahela mengi lakini unakuja kuniomba korosho zangu chache hizi, akagoma kabisa kumpa. 

Hivyo ndivyo tunavyomfanyia Mungu ndio maana hatufanikiwi tajiri ni Mungu na masikini ni sisi, fedha na dhahabu na vitu vyote viijazavyo ulimwengu ni mali ya Mungu, Mungu ana uwezo wa kufanya kitu chochote lakini anakuja lakini anachohitaji kwetu ni sehemu kidogo tu sadaka unayotoa kwa kumaanisha kama nji mojawapo ya ushirika na upendo kwake. Wengi wetu sio waaminifu kwa utoaji, je utoaji wako ni wa kumaanisha? sadaka nzuri ni ile ambayo ukitoa mpaka inakuuma rohoni.

 AINA TATU(3) ZA WATOAJI

1.WACHUKUAJI, Hawa wanapokea tu lakini huwa hawatoi Math 25:24-27, ni watu wanaopenda tu kupokea lakini hawapendi kutoa, hawachangii sehem yoyote, hawachangii hata kwny kikundi chochote hata kwenye harusi, hatoi sadaka. pia they give zero attention but theuy want full attention, hata tukisema kuna mwenzetu amelazwa tumuuombee na twende kumuangalia lakini huyu mtu hataenda hata kidogo hata kumpelekea chungwa lakini sasa yeye akiumwa atataka kila mtu aache vitu vyao waje kumuona. they are not productive at all sio kanisani wala hata kwenye jamii, ukimwambia chanhingia harusi anasema unajua sina, kunamsiba je utachangia shinganp atasema sina hata kesho sina. huwa wanaamini wao ndio wanaopaswa kusaidiwa na sio wao kusaidia. roho hii ni mbaya. takers wanalalamika sna labda kanisa lina hiv na hiv mchungaji haji kuniangalia wakat mmni mshirika wa siku nying

2.FEEDERS, hawatoi mpk wapokee hapo hapo, hawatoi mpk wawe na uhakika kwamba watapata hapo hapo na sio badae na ndomana hawatoi sana kanisani kwasababu wakitoa hawaoni jibu la papo kwa hapo. mathayo 6:1. Hawatoki kwa Mungu bali wanatoa ili kuonekana mbele za watu. wanatoa kama walipokea atachangia harusi yako kwasabbau ulimchangia yake, hawajali kuhusu mungu

3.INVESTORS, wanatoa kwanza na kupokea badae, na hapa ndio watu wa mungu tunatakiwa kuwepo math 6:19-20, ukitoa leo kwa ajili ya kanisa unaweza usione faida yake kwa sasa. hebu tuwekeze kwenye ufalme wa Mungu kwasababu hapo tu ndio kwenye uhakika ukiwekeza kwewnye mashamba mafuriko yaweza yakabeba kila kitu. Mungu hahitaji mamilion amabayo hauna bali shilingi hyo hyo uliyonayo katika mkono wako au pesa ya uwezo wako.

No comments:

Post a Comment