''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Saturday, October 15, 2016

KATIKA KILA UFANYALO MPE MUNGU NAFASI YA KWANZA ILI UFANIKIWE

Mhubiri: MCHUNGAJI ELIAS MUSSA
Maandiko: Zaburi 127:1-2; Zaburi 128:1-6; Mathayo 6:33
Zaburi 127:1-2
Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure. Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
 
Yeye ajengae nyumba yake asipokuwa na Bwana afanya kazi bure. 
Bure ina maana ya kwamba
-Hakuna Kitu(Sifuri).
-Isiyo Na maana yoyote.
 
Nyumba ina maana ya kwamba kitu chochote unachofanya wewe kama mtoto wa Mungu au Mtumishi wa Mungu. Watu kwa kuharakisha kufanikiwa wanaona Mungu si kitu na wanaangaika kuyapata mafanikio. Mafanikio bila Mungu hayana faida.
 
Zaburi 128:1-6
Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake.Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema. Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako. Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana. Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.
 
Ili kulinda mahusiano yetu tunamuhitaji Mungu kwanza katika mahusiano yetu. Danieli alitaka kuondolewa katika mahusiano yake na Mungu kwa kuwa kutungwa sheria ya kumuabudu mfalme wa nchi hiyo aliyokuwa akiishi daniel.Lakini Danieli aliendelea kumuweka Mungu kwanza nao wale wiliotunga sheria wakaenda kumshtaki lakini pamoja na yote daniel alisalimika. Daniel alisalimika kwa kuwa kwake Mungu alikuwa amepewa kipaumbele(Alimfanya Mungu kuwa wa Kwanza)
 
Mafanikio uyapatao bila kumshikisha Mungu katika jambo lote huwa si halali na hayawezi kudumu muda mrefu. Ukimpa Mungu nafasi baraka zinadondokea kwa watoto wako lakini usipompa Mungu nafasi ya kwanza Shetani Ataharibu kila jambo lililo lako na kwa familia
yako.
 
 
Mathayo 6:33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Unapomfanya Mungu wa kwanza katika kila jambo naye atajishughulisha na mabo yako yote na kuyafanya katika uweza na mapenzi yake kama apendavyo

No comments:

Post a Comment