''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, October 16, 2016

MITO YA MAJI YALIYO HAI KUTOKA MBINGUNI

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Meshark Mhini
Somo: Yohana 7:37-40, Zaburi 46:4

Yesu aliwaambia yoyote mwenye kiu sio watu fulani pekee yao bali YOYOTE mwenye KIU aje anywe, na atakaye kunywa hatahisi kiu tena. Hayo maji ni Roho Mtakatifu. Haya maji hayakauki kwasababu kuna muendelezo wa haya maji kutoka mbinguni kuja kwako. Maji haya yanavyotiririka yanakua amani, yanakupa nguvu, utawezaje kutoa mapepo kama huna Roho Mtakatifu?, huwezi ukatoa mapepo kwa nguvu zako, ni mpaka uwe na hii nguvu ya Roho Mtakatifu.
 
Ukiwa na hii nguvu ya Roho Mtakatifu utaona mambo ya ajabu mazuri yatakayo tendeka katika maisha yako. Tatizo kubwa la kanisa la sasa wameiacha hii nguvu ya Roho Mtakatifu.
 
Hii nguvu ya Roho Mtakatifu ni ya muhimu sana sana kwako. Ukiwa nayo itakusaidia kwenye kazi yako, kwenye mipango yako, ukiwa na Roho Mtakatifu utaweza kutengeneza biashara yako vizuri. Katika mwili wa binadamu; damu ni ya muhimu sana sana na ikipungua tu lazima upate matatizo, sasa ndivyo umuhimu wa Roho Mtakatifu katika maisha yako.
 
Jiulize ni kwa kiasi gani unayo hii nguvu ya Roho Mtakatifu?, Je kwa kiasi gani unaitunza hii Nguvu kwa kusoma Neno la Mungu? Je una bidii ya kusoma Neno la Mungu?, Je ukiomba unaitumua hii Nguvu ya Roho Mtakatifu?
 
Mkristo bila Roho Mtakatifu anakuwa si kitu. Usipokuwa na Roho Mtakatifu utakuwa huna hata hamu ya kuja katika ibada za kati kati na mikesha, utakuwa mtu tu wa jumapili. Ujumbe huu unakukumbusha leo ili ujichunguze mwenyewe, Je hali yako ya kiroho iko vizuri?

Maji haya yako mengi kwa Mungu ni wewe tu kuwa tayari ili mto huu utiririke ndani yako kutoka kwa Yesu mwenyewe.

Faida ya kuwa na mahusiano yaliyo hai na Roho Mtakatifu.

1. Nguvu ya kushuhudia itakuwepo, utaweza kushuudia mtaani na sehemu nyinginezo.
2. Nguvu ya kufukuza mapepo, kama huna hii nguvu utakemea masaa na masaa pepo halitatoka
3. Utapata nguvu ya kutangaza Jina la Yesu
4. Roho anatupa ujumbe wa Hekima. Mathayo 6
 
Sababu za watu wengi leo kupungukiwa hii Nguvu?
1. Watu hawana uelewa wa hii nguvu ya Roho Mtakatifu
2. Kushindwa kuvumilia wanapopatwa na majaribu
3. Kupoteza mahusiano na mawasiliano mazuri na Mungu wako, una muda wa ofisi, biashara lakini huna muda wa kutafakari Neno la Mungu.
 
Usipokuwa na Roho Mtakatifu hutaweza kuendelea sana kama ilivyotakiwa kuendelea, kwasababu baada ya kumuacha Roho Mtakatifu utakuwa unatumia akili zako mwenyewe. Kwahiyo ni kazi yako mwenyewe kila siku kuwa na kiu na hii nguvu ya Roho Mtakatifu, tamani na jitahidi kuwa nayo kila muda. Unapowaza waza ukiwa na hii Nguvu, unapoongea ongea ukiwa umejazwa hii Nguvu, unapofanya kitu fanya ukiwa ndani ya hii Nguvu.

No comments:

Post a Comment