''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, November 14, 2016

MUNGU AKISEMA KITU, HAKIKA ANAMAANISHA NA ATAFANYA ALICHOKISEMA!

Mhubiri: Mzee Kiongozi, Dr. Mumghamba
Maandiko: 2Wafalme 19:6-23,32-37


Tunaona jinsi mfalme Senakeribu wa Ashuru alivyo mtunaka mfalme Hezekia wa Yuda na Mungu wake aliye hai, kwa kusema aulize ni wafalme wangapi waliopona katika mikono yake na ya kwamba asikudanganye huyo Mungu wako kwamba wewe utaokoka. Na tunaona mtumishi wa Mungu Hezekia alipopata waraka huu ni mara ya pili anatukanwa, tunajua kwamba goliati alitunaka mwezi mzima mpaka Daudi alipo shuka kwa ndugu zake ndipo aliposikia matusi ya goliati lakini tunajua jinsi goliati alivyouawa na Daudi kwa maana alimwambia mimi nakujia kwa jina la Bwana wa majeshi.
 
Sasa hili Neno tulilosoma, Hezekia akaenda akafungua ule waraka na kuusoma mbele za Bwana, Bwana akasikia na Bwana akasema, kwa habari hiyo uliyonimba nimekusikia, huyu Senakeribu anayekutishia kwanza hataingia Yuda wala hatapiga mshale, njia ile aliyojia atarudi nayo.
 
" 2Wafalme 19:32-33 32 Basi Bwana asema hivi katika habari za mfalme wa Ashuru, Yeye hatauingia mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake. 33 Njia ile ile aliyojia, kwa njia iyo hiyo atarudi zake, wala hataingia ndani ya mji huu, asema Bwana."
 
Wakati Senakeribu amekuja na majeshi yake mengi sio watu wenye hofu bali wanaojua vita kweli kweli, wakawa wako tayari kuvamia Israel, lakini Mungu alisema Senakeribu hatakanyaga mji wa Yerusalemu wala hatapiga mshale Yerusalemu na njia liyoijia ndiyo atakayoirudia. Na kweli Mungu akafanya alichosema, usiku Mungu akatuma malaika akawaua jeshi Zima la watu mia na themanini na tano elfu, Senakeribu akaachwa ili awe shahidi, Senakeribu aliyemtishia Hezekia kwamba atafanya hiki na kile akaamka asubuhi na kukuta jeshi lake lote ni maiti tu, akageuka akarudi alipotoka akaenda kwa mungu wake(asiye hai) kujielezea na alipokuwa akiomba watoto wake aliowazaa wakaja na kumuua pale pale mbele za mungu wake, Neno la Bwana likatimia hakukanyaga Yerusalem wala hakupiga mshale, njia ile aliyoijia ndio aliyoirudia.

Kile Mungu anachokisema anamaanisha na kweli atakitenda, pamoja na vitisho vingi alivyosema Senakeribu lakini mwishoni ni kweli hakukanya Yerusalemu. Yawezekana na wewe umetishiwa vingi sana kazini kwako, shuleni kwako kwenye biashara yako, adui zako wamekutishia mengi wamekusemea mabaya mengi, au shetani mwenye moja kwa moja amekutisha mengi na kukwambia hutafika hutafanikiwa kakwambia wewe si kitu, lakini usihofu kuhusu hilo kumbuka ni nini Mungu alisema kwa ajili yako kwenye Kumbukumbu 28 alisema wewe utakuwa kichwa tu huwi mkia, utakuwa juu tu wala hutakuwa chini, na kwasababu ni Yeye Mungu aliye hai ndiye aliyesema basi hakika itatokea.

Marko 4:35 "35 Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo. 36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye. 37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? 39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. 40 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? 41 Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?"

Yesu aliwaambia na tuvuke mpaka ng'ambo alafu Yesu akalala wanafunzi wakawa na wanapiga makasia badae wakakutana na dhoruba kuu chombo kikaanza kujaa maji wanafunzi wakaanza kukata tamaa wakaamua kumuasha Yesu wakiona kuwa Yesu hajali kuwa wao wanaangamia, Bwana Yesu akaona hawa bado hawakuelewa alichokisema mwanzo akaamua aukemee upepo kwanza kukawa na shwari kuu alafu badae akawarudia kuwauliza kuhusu Imani zao. Alishasema na tuvuke mpaka ng'ambo kwahiyo ilimaanisha hata kama kutokee dhoruba kuu au kitu chochote wangefika tu ng'ambo kwasababu Yesu alishasema na akisema anatekeleza. Kulikuwa na dhoruba kuu lakini akafanya kuwa shwari kuu.

Yawezekana unavuka kwenda ng'ambo lakini ipo dhoroba kuu amini kwamba Mungu alichokisema ndicho anachomaanisha, utavuka hata kama kuna dhoruba kuu iko shwari kuu ndani ya Yesu Kristo.

Mungu anakasirika sana pale tunapokuwa hatuamini sana kile alichosema au kuchukulia kawaida kile alichosema, hata Paulo aliwauliza wagalatia ni nani aliyewaloga?, kwasababu sahivi inaonekana unapata tatizo kubwa kutokana na watu waliokwambia utakiona hutafanikiwa na ukaingiwa hofu kiasi cha kwamba wewe huna matumaini tena una wasiwasi una mashaka, lakini Bwana Yesu alisemaje nini juu yako mtumishi wa Bwana? amesema sitakupungukia wala sitakuacha kabisa, imekuwaje sasa una wasiwasi? imekuwaje sasa una mashaka? imekuwaje sasa huna matumaini? imekuwaje sasa unalalamika? imekuwaje sasa humtegemei Mungu tena? imekuwaje sasa unaenda kwa watu kuwaeleza matatizo yaliyo kusibu jinsi flani alivyokuonea?.

Hezekia alienda moja kwa moja kwa Bwana na ule waraka wa vitisho aliopewa na wewe kwanini usimwambie Bwana Yesu? Yuko Mungu ambaye atashuhulikia tatizo lako na hao wanaokusumbua hawatakusumbua tena na tatizo ulilonalo hutakuwa nalo tena. 2Nyakati 20:15 "akasema, Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; Bwana awaambia hivi, Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya Mungu."  Mungu anakwambia vita hii sio yako ni ya Bwana, sasa wewe una vita  sasa kwanini ufanye vita kuwa vyako?, Kutoka 14:14 "Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya". Bwana hapendezwi na mtu mwenye mashaka mwenye kusitasita, Waebrania 10:38 "Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye". Amini kuwa kile alichokisema Mungu atakifanya maishani mwako. Mungu sio mwanadamu hata aseme uongo. Mungu aliwakasirikia wana wa Israel akawaambia mtanidharau mpaka lini kwanini wanazani Mungu hataweza kuwaingiza Kanani kwasababu walijiona watu wa kanani ni wakubwa wao ni kama panzi mbele yao kasoro Joshua na Kalebu, lakini badae waliweza kuingia Kanani kwasababu walikuja kumwamini kuwa Bwana anaweza. Kwahiyo na wewe mtegemee Yesu hakika utashinda hali yoyote unayopitia

No comments:

Post a Comment