''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, April 2, 2017

KUKAA KARIBU NA MUNGU

Mhubiri: Mr. Leandri Kinabo
Maandiko: Warumi 12:11, Waebrania 4:16;11:6

Kumwamini Mungu ni kitu kimoja na kuendelea kuwa karibu na Mungu ni kitu kingine au ni hatua nyingine. Watu wengi wanaamini kuwa Mungu yupo na mambo ya Yesu lakini sio wote ambao wako karibu na Mungu. Ni kweli tunamwamini Mungu lakini Je tunajileta karibu na Mungu?. Ndio unaweza ukawa na bidii ya kuja kanisani kila jumapili lakini haimaanishi kuwa uko karibu na Mungu. Warumi 12:11, inawezekana ukawa unajua mambo mengi kuhusu Yesu lakini usiwe karibu na Yesu. Kuja kanisani ni vizuri lakini kuja karibu na Mungu ni vizuri zaidi, hatoshi tu kujua Neno la Mungu na kumwamini lazima uwe karibu nae Mungu.

Warumi 12:11 "kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana"

Inatakiwa kila siku uwe na bidii ya kumjua Yesu. Ili tuwe karibu na Mungu ni lazima ufanye yafuatayo:

1. Kaa mbali na dhambi, dhambi inakutenganisha wewe na Mungu, dhambi ni adui yako mbaya sana. 
2. Lazima usamehe, hata kama mtu amekuuthi kiasi gani jitahidi kumsamehe.
3. Kutumia muda wako kusoma Neno la Mungu na kuomba kwa bidii na kwa kumaanisha.
4. Kushiriki ibada kwa uaminifu, unapokuja ibadani utamsifu Mungu, utasikia Neno la Mungu na utaenda kulitafakari na hiyo itakusaidia kuendelea kuwa karibu na Mungu.

     Waebrania 10:25 "wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia."

No comments:

Post a Comment