''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Thursday, May 25, 2017

IMANI KWA MUNGU

Mhubiri: Mr. Elisha Suku
Maandiko: Waebrania 11:1-6

Ni lazima uwe na imani kwasababu kila kitu kutoka kwa Mungu kinategemea imani, na maisha yetu kama wakristo hatuiishi kwa kutegemea tunavyoviona kwasababu Mungu wetu hawasiliani na sisi macho kwa macho bali kwa imani kwahiyo maisha yetu yanategemea sana imani. Tunapokea ahadi alizo zuahidi Mungu kwa njia ya imani, tunapokea kwasababu tu ya imani, tunauhakika wa kupokea Mungu alichokiahidi kwasababu tunaamini kwamba ni chetu na tutapokea. 

Ukimuomba Mungu kitu unapokea kwasababu tu umeamini kwamba kitakuwa chako au kitatokea. Unamuomba Mungu kitu ninakuhakikishia kama utaendelea kuamini kwamba atakupa hicho kitu na kweli utapokea. Mungu anaweza kila kitu ni wewe kuamini tu

Katika mstari wa pili (Ebr 11:2) Mungu anawasema wale mababa wa imani, sasa jiulize kwanini awakumbuke? ni kwasababu watu wale walimuamini na kuwa na uhakika na Mungu. Mungu anakuangalia wewe je uko tayari kupokea ahadi zake, anangalia je una imani, tunahitaji kuishi kwa imani. 

Bila imani hatuwezi kumpendeza Mungu. Hutakiwi kuwa imani nusu nusu, sio swala hili unamwamini Mungu na swala jingine unaamini akili zako mwenyewe. Ukimwamini Mungu lazima uendelee. Imani ni zawadi kutoka kwa Mungu, na Mungu hakufanya hii zawadi kuwa ni ya watu flani tu mpaka watu wengine wakose na wengine wapate bali ni ya wote ni wewe tu kuitumia imani. Warumi 10:8-11,13,17. 

Kwahiyo siku zote unatakuwa kuwa imani ndani mwako. Mungu yupo kwa ajili yako anasubiri tu umwamini, na pale unapo mwamini tu anaanza kutenda kazi ndani mwako. Waebrania 11:8-19 Abraham alimwamini Mungu na Mungu akampa ahadi zake. Mathayo 15:21-28 kwahiyo sio swala la mara moja au mara mbili bali ni swala la kuendelea kumwamini Mungu siku zote na muda wote, na mtazame Mungu tu, ni Mungu tu anayeweza kukupa unachotaka hata kama itachukua muda kiasi gani wewe tulia kwa Mungu wewe endelea tu kuomba kwa bidii. Usizunguke zunguke mara unaenda kwenye kanisa hili na hili, Yesu tu ndiye mwenye jibu la uhakika endelea kung'ang'ania kwa Yesu na Yesu atajibu ombi lako muda wowote mahali popote. Marko 11:21-25 ukiamua kumwamini Mungu kwahiyo ni uamuzi, ukiamua kumwamini Mungu utapokea ahadi za Mungu. Mungu ana mpango mzuri sana kwa ajili yako wewe mwamini tu.

No comments:

Post a Comment