''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, May 14, 2017

TAMAA JUU YA MAFANIKIO YA VITU, HULETA HASARA YA DAIMA

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: 2Wafalme 5:15-27

Naamani alivyopona baada ya kutii alichoambiwa na Elisha, Naamani akataka kumpa zawadi nyingi Elisha kana kwamba Elisha ndio aliyefanya ule muujiza. Lakini Elisha alimwambia Naamani arudi na vitu vyake, Elisha alimwambia vile sio kwasababu alikuwa na vitu vingi bali ni kwasababu anajua kwamba mpomyaji sio yeye bali ni Mungu. sasa Gehazi mtumishi wa Elisha alishazitamani zile zawadi jinsi zilivyokuwa nzuri na za kuvutia, na akawa anashangaa kwanini  bwana wake amezikataa, na tamaa ile ikamfanya amkimbilie Naamani baada ya kuondoka, na baada ya kumpata huko njia Gehazi akaamua kusema uongo kwa Naamani ili apate zile zawadi. Kwahiyo hapa tunagundua kwamba tamaa inaweza kukuletea dhambi nyingine ya kudanganya ili upate kile unachokitaka kwa njia isiyo halali. Gehazi akajua bwana wake Elisha hatagundua, kumbe roho ya Elisha iliinda nae na alijua kila kitu alichofanya, na akamlaani ukoma wa Naamani ukamrudia Gehazi.

Jamani tamaa ni mbaya, leo hii unakuta mtu wa Mungu una madeni mengi kisa unataka ununue hichi na hichi ambacho huna uwezo nacho, sasa mtu anayekudai akikunyanganya vitu vyote huo si ndo ukoma!. Tamaa ya vitu ni mbaya sana, kwanini utamani vitu ambavyo huna uwezo navyo yule ana gari na wewe unataka gari au yule ana nyumba nzuri na wewe unataka uwe nayo, unatamani kiasi kwamba unatumia njia zisizo halali. Hapana acha tamaa mbaya, hivyo vitakuja kwa muda wake, wapendwa mnadaiana mpaka hamuwezi kusalimiana. 

Kwanini usisubiri, leo hii unatembea kesho Mungu atakupa gari mbio za nini?, usikimbilie ukoma kama Gehazi, sawazisha fanya marekebisho. Hata wenye vyeti feki ni kwasababu ya tamaa, unaona mwenzako yupo mahali flani unaona ufoji ili na wewe ufikie hapo.

 Ndugu rizika na ulicho nacho afadhali kula matembele lakini unalala kwa amani, kuliko kula nyama na kupata ukoma. Unataka vitu vya ghali alafu ukoma unakupata. Fanya juhudi katika mema, usitamani mafanikio ya haraka haraka na kuamini makanisa ya uongo, mwaminini Mungu, Mungu ndio mwenye uwezo wa kukufanya tajiri na sio kukanyaga mafuta. Pale kazini usidanganye fanya haki sema ukweli, mtu akisahau chenji yake mrudishie usiseme 'mungu anipe nini tena', uwe mwaminifu hata kufa Bwana atakupa taji ya uzima, jiepusha na mambo yasiyo ya haki. 

Mpendeni Mungu acheni tamaa acha dhuluma, usitamani vitu visivyo vya kwako. Ukifanya mali za udhalimu Mungu anaipukutisha yote! yote!. Anza na Mungu atakupa mali kwa muda muafaka na kwa haki. Mafanikio yanayoletwa na tamaa ni hasara kubwa sana. Futa hiyo na uanze na Bwana sasa. Yawezekana mtu wa Mungu bila kujua ukapata kitu kisicho halali ulitumia ujanja mwingi ukapata mali uliyonayo, sasa tubu kwa Mungu mwambie bwana nilikosa nilikimbilia mali ile kwa tamaa na sasa umepata ukoma, mwambie Bwana umekosa unahitaji akusamehe, ee Bwana usiniue nirehemu. Yuda tamaa yake ilimuondoa. heri leo usikie sauti ya Mungu usiendelee kupotea, Akani kwasababu ya tamaa alipata laana ya kizazi na kizazi.

No comments:

Post a Comment